Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shaka: Rais Samia anairejesha CCM kwenye zama za ujmaa, kujitegemea
Habari za Siasa

Shaka: Rais Samia anairejesha CCM kwenye zama za ujmaa, kujitegemea

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

 

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, amesema Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan sasa anakirejesha Chama kwenye zama za ujamaa na kujitegemea kama ilivyoasisiwa na viongozi wa taifa wakiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruangwa … (endelea).

Alisema hayo jana Jumanne tarehe 31 Mei 2022 aliposhiriki ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Namichiga, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na uhai wa chama ambapo alieleza kufurahishwa kwake na ushiriki wa wananchi katika ujenzi huo kwa kujitolea.

“Mwenye kokoto, mwenye simenti, mwenye kila kitu tunakwenda kuunga nguvu ujenzi wa taifa ili kufikia maendeleo kwani hatuna mjomba, hatuna shangazi, hatuna mama mdogo atakayetoka anakotoka aje atufanyie kazi ya kujenga maendeleo kwa umoja wetu, mchango wetu ni muhimu ili chama hiki kuhakikisha kimesimama.”

“Wazee wetu walifanya haya tunayoyafanya sisi (kujitolea nguvu). Nimefarijika sana na kinamama mnavyotisha katika kushika hatamu za kuongoza nchi kama ambavyo Rais Samia anafanya, lakini mnatisha kwenye kuhamasisha maendeleo,” alisema Shaka

“Wakinamama kwenye ujenzi wamekuwa wengi zaidi, kwenye uhamasishaji wamekuwa wengi zaidi, kwenye kutuongoza wanafanya vizuri zaidi kama anavyofanya Rais Samia, Mungu awabariki sana, Mungu awalinde sana mama zetu kwa namna ambavyo mnaleta ari na shime ya maendeleo kwenye taifa hili,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan

Kuhusu kasi ya maendeleo, Shaka alisema yako pale pale na kwamba kutokana na kutambua mchango wa wakulima serikali ya awamu ya sita itaendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo ili ilete tija kwa kila mkulima nchini.

Alisema anatambua huko nyuma kulikuwa na changamoto katika kilimo cha zao la korosho, lakini serikali chini ya Rais Samia imeendelea kuzitafutia ufumbuzi.

Kwa mujibu wa Shaka, miongoni mwa utatuzi wa changamoto hizo ni pamoja na kutoa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima wa korosho ambazo zitagawiwa bure kwa wakulima wa zao hilo.

“Nipongeze mpango wa serikali wa kutoa pembejeo bure kwa wakulima, Rais Samia anafanya maendeleo bila kubagua na bahati nzuri Mbunge wenu (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) naye anafanya kazi nzuri ya kuhakikisha anawatetea wananchi wa Ruangwa.

“Serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Rais Samia itaendelea kutatua changamoto na kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuongeza fedha za maendeleo katika kila sekta mfano mzuri nimeelezwa hapa Wilaya ya Ruangwa huko nyuma ilikua inapata shilingi milioni 400 kwa ajili ya miradi ya barabara, lakini sasa imepokea zaidi ya shilingi bilioni 1.5, hakika chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kazi inaendelea tena kwa kasi kubwa,” alisema.

1 Comment

  • Asante ndugu shaka ccm ndio chama tawala sisi wapiga kura wenu hatuoni faida ya baadhi ya wa kuu wa wilaya sisi wapiga kura wenu hatuoni faida ya baadhi ya wa kuu wa mikoa sisi watu wa daraja la tatu tumekuwa kama wafiwa malalamiko yetu ni kilio

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!