Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu vita na Urusi
Kimataifa

Marekani kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu vita na Urusi

Spread the love

MAREKANI itaitumia Ukraine mifumo ya juu zaidi ya roketi kuisaidia kujilinda, Rais Biden ametangaza.

Kwa mujibu wa BBC silaha hizo, zilizoombwa kwa muda mrefu na Ukraine, ni kusaidia kushambulia vikosi vya adui kwa usahihi kutoka umbali mrefu.

Hadi sasa, Marekani ilikuwa imekataa ombi hilo kwa kuhofia silaha hizo zinaweza kutumika dhidi ya shabaha nchini Urusi.

Lakini siku ya Jumatano, Bw Biden alisema msaada huo utaimarisha msimamo wa Kyiv wa mazungumzo dhidi ya Urusi na kuleta suluhu la kidiplomasia zaidi.

Akiandika katika gazeti la New York Times, alisema: “Ndiyo maana nimeamua kuwa tutawapa Waukraine mifumo ya juu zaidi ya roketi na zana ambazo zitawawezesha kushambulia kwa usahihi shabaha muhimu kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine.”

Silaha mpya zitajumuisha Mfumo wa Roketi wa Kivita wa M142 (HIMARS), afisa mkuu wa Ikulu ya White House alisema – ingawa hakufafanua ni ngapi kati yao zitatolewa.

Mifumo hiyo inaweza kurusha makombora mengi ya kuongozwa kwa usahihi katika shabaha hadi kilomita 70 (maili 45) – mbali zaidi kuliko mizinga ambayo Ukraine inayo sasa hivi. Pia inaaminika kuwa sahihi zaidi kuliko silaha za Urusi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!