SERIKALI imetenga Sh. 500 milioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwaajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta safi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hayo yamebainshwa na Waziri wa Nishati, Januari Makamba leo Jumatano tarehe 1 Juni, 2022 akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Makamba amesema kazi zitakazofanyika ni kufanya mapitio ya nyaraka za mradi; kuanza taratibu za kumpata Mshauri Mwelekezi wa kufanya Upembuzi Yakinifu wa mradi pamoja na Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii zitokanazo na utekelezaji wa mradi.
Waziuri huyo amesema bomba hilo lenye urefu wa takribani kilomita 1,710 litatumia mkuza wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la TAZAMA.
Aidha amesema Bomba litamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia.
Leave a comment