Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Shabiki stars apoteza maisha uwanjani, Tff watoa neno
Michezo

Shabiki stars apoteza maisha uwanjani, Tff watoa neno

Spread the love

Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Tff, Wilfred Kidau ametoa pole kwa familia ya shabiki mmoja aliepoteza maisha kwenye mchezo wa kufuzu kombe la Dunia 2022 kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi, kwa mshituko wa moyo baada ya Burundi kusawazisha bao  katika kipindi cha kwanza. Anaripoti Martin Kamote… (endelea)

Kidau ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam na kusema kuwa ‘ni mtu ambae ni shujaa na mara baada ya mkutano huu na wandishi wa habari kuisha, nitatoa  maelekezo ofisini wanitafutie hio familia inapokaa angalau kama tff tutaenda kujumuika na  wenzetu kwenye kipindi hiki kigumu, mtu ambae ametangulia mbele za haki akiwa kwenye kulipigania taifa ni jambo kubwa sana na sisi tuwape pole,

Aidha ameongeza kwa kumpongeza haji manara kwa kazi kubwa alioifanya chini ya kamati yake ya hamasa ambayo ni kamati ndogo ya ushindi wa taifa stars , alifanya jambo kubwa akiwa na wasanii mbalimbali kuelekea kwenye mechi hii na kamati kubwa ya saidia taifa stars ishinde  inayoongozwa na mwenyekiti ambae ni mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda

Pia ameipongeza serikali kupitia wizara yenye dhamana ya michezo na mhe waziri mwenyewe dkt halson mwakiyembe kwa kazi kubwa.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa na EURO hapa Meridianbet

Spread the love  Baada ya jana kushuhudia mechi kali ya ufunguzi wa...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

error: Content is protected !!