Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yawapa unafuu wakaazi Magomeni Kota
Habari za Siasa

Serikali yawapa unafuu wakaazi Magomeni Kota

Spread the love

 

SERIKALI imewapa unafuu wakaazi wa nyumba mpya za Magomeni Kota kwa kuwawezesha kununua nyumba hizo kwa mfumo wa mpangaji mnunuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Nafuu hiyo imetolewa na Rais Samia Suluhu leo Jumatano Tarehe 23 Machi 2022, wakati akizundua nyumba hizo na kukabidhi funguo kwa kaya 644.

Wakaazi hao kwa mujibu wa makubaliano wataishi katika nyumba hizo kwa miaka mitano bure ili kufidia gharama walizotumia kuishi nje ya makazi yao baada ya nyumba zao kubomolewa.

Hata hivyo, Rais Samia amewashauri wakaazi hao kuanza kulipa fedha hizo kidogo kidogo kuanzia sasa badala ya kusubiri miaka mitano ili kupunguza mzigo.

Mbali na nafuu hiyo ya ununuzi pia Serikali imewapa muda wa mapumziko ya kutochangia huduma kwa kipindi cha miezi mitatu.

Amewataka wakaazi hao kuzitunza nyumba hizo kwa kuzingatia usafi wa maeneo yanayowazunguka ili ziweze kudumu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!