Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanaosema miradi haitaendelezwa wana upeo mdogo: Samia
Habari za Siasa

Wanaosema miradi haitaendelezwa wana upeo mdogo: Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema watu wanaofikiri kwamba miadi iliyoachwa na mtangulizi wake haitaendelezwa wana upeo mdogo wa kufikiri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 23 Machi 2022, akizundua nyumba za Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.

Amesema waliokuwa wanasema hivyo hawakuwa hata na sababu na kubainisha kuwa hakuna sababu ya miradi kutoendelea kwasababu imeagizwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Serikali zote zinazoongoza Tanzania ni za Chama Cha Mapinduzi awamu moja ikiondoka awamu ya pili inashika Serikali… kwahiyo wanaposema kwamba miradi haitatekelezwa nadhani upeo wao wa kufikiri ni mdogo sana,” amesema na kuongeza;

“Hata miradi hii ilivyoanzishwa awamu ya tano mimi nilikuwa Makamu wa Rais kwahiyo ni sehemu ya miradi hiyo kuanza kwake na kutekelezwa kwake.

“Lakini kwa kunitazama sura na kusema asingeweza kuendeleza hii miradi haikuwa busara, lakini tuwaombee nasi tujiombee Mungu atupe nguvu na busara zaidi miradi hii iendelee kwa maendeleo ya nchi yetu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!