Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yataka ushirikiano na NGO’s
Habari Mchanganyiko

Serikali yataka ushirikiano na NGO’s

Spread the love

 

SERIKALI imetaka ushirikiano na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini (NGO’s), katika uwasilishaji wa masuala yanayohusu Tanzania, kwenye mikutano ya kimataifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa jana tarehe 7 Machi 2022, jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene, wakati akizungumza na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), juu ya namna ya kuboresha mifumo ya utoaji haki nchini.

Simbachawene ametoa wito huo akizungumzia maandalizi ya ujumbe wa Tanzania, kwenda Geneva nchini Uswis, kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo ya Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa (UN), kuhusu haki za binadamu, iliyokubali kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

“Tutakwenda huko tukiwa kitu kimoja na hivi karibuni tunapojiandaa kwenda kwenye mkutano Geneva, nitaongoza deligation ya Serikali. Kama kuna lolote tunaweza badilishana, kama kwa upande wenu kuna watu wanaokwenda ni vizuri tukakaa pamoja tukazungumza tukasimamie jambo gani,” amesema Simbachawene.

Pia, Simbachawene amezitaka NGO’s kufanya mazungumzo na Serikali kabla ya kwenda kuwasilisha masuala yanayoihusu nchi katika mikutano ya kimataifa.

Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene

“Yako baadhi ya maeneo ambayo mmeyagusa, kama hili la ushiriki kwenye international forums (majukwaa ya kimataifa), hili tutajitahidi sana tunapotaka kutoka tufanye pre-meetings (mikutano ya awali) kabla hatujaondoka ili asitokee mtu anaongea kama vile yeye hii nchi ataondoka kesho,” amesema Simbachawene.

Aidha, Simbachawene amewaomba wadau wa NGO’s kutowasilisha mambo yanayoiabisha nchi katika mikutano ya kimataifa.

“Nilienda kwenye mkutano wa mazingira nchi ya nje, tukawa na Mtanzania ambaye wenzake hata tunapokaa wa Serikali hataki hata kukaa, kuzungumza na salamu na sisi hataki. Halafu tuko nchi ya watu,” amesema Simbachawene na kuongeza:

“Bahati mbaya sana alipokwenda kuzungumza masulaa ya mazingira kama vile amekwenda kutushtaki hatustahili kupewa fedha kwa ajili ya kutunza mazingira. Kimsingi mambo kama hayo yanapojitokeza ni aibu ya nchi wala sie yeye wala sio sisi. Sababu Serikali ni mfumo, sisi tunakuja tunapita wanakuja wengine.”

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu Taifa

Katika mkutano huo, THRDC iliwakilishwa na Mratibu wake, Onesmo Ole Ngurumwa. Jaji Mstaafu Joacquine De Melo (Mwenyekiti wa Bodi THRDC). Hassan Juma (Mjumbe wa Bodi ya THRDC), na Jaruo Karebe (Mratibu wa THRDC Kanda ya Kati).

Mtandao huo ulimfikishia mapendekezo sita Simbachawene, ambayo ameahidi kuyafanyia kazi.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni, wizara kuweka utaratibu mzuri wa kutambua na kuripoti kazi zinazofanywa na watetezi wa haki za binadamu pamona na kufanya maboresho kwenye maeneo ya utoaji msaada wa kisheria na mifumo ya utoaji haki nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!