MAMLAKA nchini Benin imemwachia huru kiongozi wa Nigeria anayetaka kujitenga, Sunday Lgboho Adeyemo kulingana na msemaji wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Lgboho alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Benin julai 2021 pamoja na mkewe , kwa ombi la Nigeria ingawa mkwewe aliachiwa siku chache baadae. Wanandoa hao walisemekana kuelekea Ujerumani ambako mkewe ni raia wa huko.
Alishitakiwa kwa kuingia Benin kinyume cha sheria nakupanga kuleta fujo , lakini halikanusha mashitaka hayo. Mamlaka ya Nigeria haikuwai kutoa ombi rasmi la kurejeshwa kwake nchini mwake .
Katika taarifa zake siku ya Jumatatu msemaji wake alisema Lgboho aliachiwa na kiongozi wa shirika la Mwamvuli makundi ya kujitawala ya Yuruba, Banji na Akintoye.
Leave a comment