Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BAWACHA yawapa jukumu wanawake
Habari za Siasa

BAWACHA yawapa jukumu wanawake

Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge
Spread the love

 

BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), limewataka wanawake kujenga familia zinazozingatia misingi ya usawa wa kijinsia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 8 Machi 2022 mkoani Iringa na Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge, katika kongamano la BAWACHA, la kuadhimisha siku ya mwanamke duniani.

Ruge amesema ili vitendo vya ukatili wa kijinsia vitokemezwe, wanawake wanawajibu wa kujenga jamii isiyo na ubaguzi.

“Ssisi kama wanawake tuna wajibu kuhakikisha tunajenga jamii isyo na ubaguzi na dunia jumuishi, sababu sisi ni mama tunazaa watoto, tuna wajibu kuweka hiyo mindset ya usawa wa kijinsia toka tunalea watoto wetu tangu wadogo,” amesema Ruge.

Ruge amesema “huu ujumbe muufanyie kazi sababu mara nyingi tumekuwa tukilalamika wanaume wanatukandamiza, lakini hawa wanaume tumewazaa sisi. Kwa hiyo tunawajibu wa kuhakikisha tunakwenda kujenga familia ambayo ina usawa wa kijinsia.”

Aidha, Ruge amewataka wanawake kuacha mazoea, bali wawe na uthubutu wa kufanya vitu ambavyo wanahisi viko nje ya uwezo wao.

“Lakini pia tuache kufanya vitu vya mazoea, kina mama tutoke kwenye confort zone na tufanye mambo ambayo tunayaogopa. Lile unalofikiriaa siwezi ndiyo unatakiwa ulifanye, zile ndoto kubwa kubwa ndiyo unatakiwa uziote na uzitimize na hata yale mambo tunayofanya kila siku, basi tuyafanye kwa ubora zaidi,” amesema Ruge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!