Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yamwaga ajira sekta ya Afya
Afya

Serikali yamwaga ajira sekta ya Afya

Waziri wa Muungano, Suleiman Jafo
Spread the love

SERIKALI imetoa ajira mpya za watumishi kada za afya katika Mamlaka za serikali za Mitaa  (TAMISEMI) 6180 kwa mwaka wa fedha 2018/19. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma,  Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa  na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo amesema ajira hizo ni utekelezaji wa  ahadi ya serikali katika kuboresha huduma ya afya.

Jafo amesema kuwa ajira zao zimetokana na kibali kilichoandikwa kwa serikali cha kuajili watumishi wa kada mbalibali wa sekta ya afya nchini.

“Kibali hiki ni mwendelezo wa kibali cha ajira kwa kada za afya 3152 kilichotolewa mwezi Julai 2017 kwa lengo la kukabiliana na changamoto za utumishi katika vituo vya afya nchini.

“Napenda kiwataarifu kuwa serikali imekamilisha mchakato wa ajira ya watumishi 61,800 wa kada mbalibali za afya ikiwemo madaktari, wafamasia, wataalamu wa maabara, wauguzi, utabibu wa huduma wa afya na wataalamu wengine wa sekta ya afya ambapo watumishi hao wamepangwa katika Manlaka za serikali za Mitaa zote ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za afya nchini,” amesema Jafo.

Aidha amesema zipo baadhi ya kada zilizokosa waombaji wenye sifa kuwa ni,wahandisi wa vifaa tiba, maofisa wauguzi ngazi ya shahada, wataalamu wa mionzi, madaktari wa meno na wataalamu wa viungo bandia.

“Nawashauri wananchi kusomea taaluma hizo kwani mahitaji ni makubwa mno katika vituo vya kutolea huduma nchi,” amesema Jafo.

Jafo amesema kuwa mgawanyo  wa watumishi umezingatia halmashauri zenye hospitali,vituo vya afya na zahanati zilizokamilika lakini zilikuwa hazifanyi kazi ipasavyo kwa kukosa watumishi.

Amesema kuwa mgawanyo umezingatia vituo vya afya 210 vilivyoboreshwa katika halmashauri mbalimbali ili kuziwezesha kutoa huduma zilizokusudiwa.

Hata hivyo Jafo ametoa wiki mbili kwa watumishi waliochaguliwa kuwa wameisha fika katika vituo vyao vya kazi na kama kuna mtu ambaye atafika katika kituo chake cha kazi ndani ya siku 14 nafasi yake atapewa mtu mwingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

Afya

LHRC yapinga kufutwa Toto Afya: Ni ukiukaji wa sheria za watoto

Spread the love  KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa...

Afya

Manesi 7 mbaroni tuhuma za kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane

Spread the love  JUMLA ya wauguzi/manesi saba wa Hospitali ya Manispaa ya...

error: Content is protected !!