Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yamsulubu Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yamsulubu Mbowe

Jengo la Bilicanas linavyoonekana kwa juu baada ya kubomolewa
Spread the love

SERIKALI ya Rais John Magufuli imemmaliza Freeman Mbowe katika biashara yake ya klabu (Billicanas), anaandika Faki Sosi.

Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ameng’olewa rasmi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwenye jengo ambalo alikuwa ameweka biashara zake.

Mbowe aliweka biashara ya klabu (Billicanas) na uzalishaji wa gazeti lake la Tanzania Daima chini ya Kampuni ya Free Media kwenye jengo hilo lililopo katika makutano ya Barabara ya Mkwepu na Indira Gandhi kitalu namba 725-726/24 kilicho na hati namba C.T No. 186018/15 na C.T No. 186018/10.

Leo ni siku ya pili baada ya NHC kuanza kubomoa jengo hilo wakati ambao Mbowe akiwa kwenye mgogoro na shirika hilo la serikali pamoja na Kampuni ya Udalali ya Poster and General Traders baada ya kuondoa vyombo vya kampuni hiyo nje Septemba mwaka jana kwa madai ya kudaiwa Sh. 1.2 bilioni ikiwa ni deni la miaka 20 la pango hilo.

Ubomoaji huo unafanywa chini ya ulinzi mkali huku Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa NHC akieleza kuwa, ubomoaji huo utadumu kwa siku tatu na kwamba, kuna uwekezaji mkubwa unaotaka kufanywa kwenye eneo hilo.

Hatua ya kuondolewa vyombo vyake kwenye jengo hilo kulisababisha Mbowe kwenda katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kufungua kesi dhidi ya hatua hiyo na kuweka pingamizi.

Katika kesi hiyo namba 722 ya mwaka 2016, Mbowe aliwakilishwa na mawakili na Peter Kibatala na Omary Msemo ambapo NHC iliwakilishwa na mawakili wake Aloyce Sekule na Miriam Mungula.

Mbowe alidai mahakamani kuwa, yeye na shirika hilo walikubaliana kwamba, alikarabati na kulipanua jengo hilo kwa gharama zake kwa asilimia 100, makubaliano ambayo waliyaingia mwaka 1997.

Katika makubaliano hayo, Mbowe alidai kuwa walikubaliana kumiliki jengo hilo kwa pamoja kwa muda wa miaka 99, huku yeye akitakiwa kupata asilimia 75 katika mgawanyo wa mapato na NHC ikitakiwa kupata asilimia 25.

Hivyo alidai kuwa hatua ya NHC kumtoa kwenye jengo na kuchukua mali zake ni kuvunja mkataba huo. Mbowe aliondolewa kwenye jengo hilo mnamo Septemba Mosi mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!