August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ander Herrera kutembelea Tanzania

Ander Herrera

Spread the love

KIUNGO wa Manchester United na  Hispania, Ander Herrera anatarajiwa kutembelea nchi mbili zilizopo kwenye Ukanda wa Afrika ya Mashariki ikiwemo Tanzania bila kuweka wazi sababu zitakazomfanya kuja  wala kutaja muda gani atakaotua nchini.

Herrera ameandika haya kwenye ukurasa wake mtandao wake wa Twitter baada ya kuulizwa swali na moja ya mashabiki zake, Je ni sehemu gani ya dunia unayopenda kutembea na lakini haujawahi kuwa awali?

Kiungo huyo alitaja nchi nne ambazo ana mpango wa kuzitembelea kwa siku za hivi karibuni lakini katika Ukanda wa Afrika Mashariki anatamani kutembelea Kenya na Tanzania, na nyingine zikitokea America ambazo ni Colombia na Argentina.

Tamaa ya mchezaji huyo kuja nchini, huwenda ikawa imechagizwa na ziara iliyofanywa na magwiji wa klabu ya FC Barcelona waliokuja nchini Machi 28, 2015 na kutembelea vivutio vya ndani baada ya kucheza mchezo katika uwanja wa Taifa dhidi ya Maveterani wa Tanzania.

error: Content is protected !!