Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yafafanua kuondolewa dawa 178 kitita cha NHIF
AfyaTangulizi

Serikali yafafanua kuondolewa dawa 178 kitita cha NHIF

Spread the love

SERIKALI imesema imeondoa dawa 178 katika kitita cha Mfuko wa Taifa wa Bima (NHIF), ili kupisha dawa bora zaidi zinazoendana na wakati wa sasa kwa magonjwa yote yanayowakumba watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ufafanuzi huo umekuja siku chache baada ya kuibuka vute ni kuvute kuhusu matumizi ya kitita hicho kilichohuishwa tarehe 18 Disemba mwaka jana na kupingwa na baadhi ya wamiliki wa hospitali binafsi.

Akitoa ufafanuzi leo Jumamosi Mkurugenzi wa Huduma za Dawa na Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi amesema baadhi ya dawa hizo zimeondolewa katika muongozo huo wa matibabu ili kuepuka uandishi wa dawa zenye muunganiko yaani Fixed Dose Combonation kwa kuwa nyingi zinakuwa zimebeba majina ya kibiashara.

Amesisitiza kuwa mwongozo huo umezingatia upatikanaji wa dawa zote muhimu kwa magonjwa yote nchini na kwa ngazi zote kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Baadhi ya dawa zilizoondolewa ni zile zinazotibu magonjwa ya presha na sukari na wenye matatizo ya moyo.

Dawa za malaria kadhaa aina ya Artemether za vidonge, sindano na dripu pia zimeondolewa kwenye kitita hicho pamoja na dawa ya vidonge ya chloroquine inayotibu wenye selimundu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!