Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali yaahidi kuzilegeza masharti shule binafsi
Elimu

Serikali yaahidi kuzilegeza masharti shule binafsi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda
Spread the love

 

SERIKALI imeahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa wamiliki wa shule binafsi, ili ziweze kutekeleza majukumu yake vizuri ya kutoa elimu bora kwa watanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 10 Oktoba 2023 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, katika kikao chake na wamiliki wa shule binafsi, baada ya kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye uendeshaji.

Waziri huyo wa elimu amesema kuwa, shule binafsi sio adui wa serikali bali ni mdau katika maendeleo ya elimu nchini.

“Na sisi tutajitahidi kuwaonyesha nyie tunawahitaji sana, tutafanya kazi pamoja sababu nyie ni wadau bila nyie tusingekuwa hapa. Ni rahisi kusahau kuna wakati shule zinafunguliwa tunaona mabasi yanakimbia kwenda Nairobi na Kampala, watu wanapeleka watoto wao nje ya nchi kiutafuta elimu matokeo yake wanakuwa mbali na watoto,” amesema Prof. Mkenda.

Amesema “baada ya sekta binafsi na taasisi za dini kuongeza uwekezaji kwenye elimu, wazazi sasa wana uchaguzi wanasomesha watoto hapa hapa Tanzania.”

Prof. Mkenda amesema Serikali ya Rais Dk.. Samia Suluhu Hassan, imejipambanua kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu.

Moja ya changamoto kubwa inayolalamikiwa na wamiliki wa shule binafsi, ni kodi na tozo mbalimbali, ambapo wameiangukia Serikali na kuiomba izipunguze ili waweze mudu gharama za uendeshaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!