Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Tusibweteke Corona bado ipo
Habari Mchanganyiko

Serikali: Tusibweteke Corona bado ipo

Spread the love

WAKATI baadhi ya wanajamii wakionesha kutokuwa na kumbukumbu kwa kilichotokea mwaka 2020 baada ya kuibuka kwa maradhi mapya ya UVIKO – 19 na kusababisha baadhi ya watu kupoteza maisha, Serikali imekumbusha ugonjwa huo bado upo na watu wazidi kuchukua hatua ya kujikinga na maambukizi mapya. Anaripoti Marry Victor, Dodoma… (endelea).

Kwa mujibu wa ripoti Shirika la Afya Duniani (WHO) ya hivi karibuni idadi ya visa vipya kuanzia  tarehe 23  hadi 29 Julai, 2022 Kanda ya Western Pacific ni asilimia 52, Eastern Mediterranean  asilimia 45 na Southern Eastern Asia ni asilimia 13.

Ripoti hiyo imeendelea kubainisha kwamba kwa upande wa Afrika  jumla ya visa  ni 9,209,133, visa vipya ni 17,227, vifo ni 173,974, vifo vipya kwa siku saba zilizopita ni 32.

Akichambua ripoti hiyo, Afisa wa kitengo cha Elimu kwa umma na Ushirikishaji jamii wakati wa dharura, Juliana Mashama alisema kama ilivyo kwa mataifa mengine Tanzania imepitia mawimbi manne ya UVIKO_ 19 huku akisisitiza malengo ya nchi katika kudhibiti maambukizi mapya ya maradhi hayo.

“Lengo kuu la nchi ni kutoa chanjo kwa angalau asilimia 70 ya Watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ifikapo Desemba 2022.

Kwa mujibu wa Juliana idadi ya dozi zilizopokelewa nchini ni kiasi cha 2,4376,529 sawa na asilimia 99 tayari zimesambazwa. Dozi iliyotumika mpaka kufikia tarehe 14 Agosti, 2022 ni 21,370, 545.

Kwa mujibu wa Juliana hali ya ufikiaji malengo ya uchanjaj ikiwa ni watu 21, 528, 650 wawe wamepatiwa chanjo ya UVIKO – 19.

Akitoa taarifa yake kwa wananchi Jijini Dodoma hivi karibuni, Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Aifello Sichalwe amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na UVIKO -19 kwa kupata wakati dozi kamili za chanjo ya UVIKO -19.

“Kuvaa barakoa pindi unapojisikia dalili za nafua na kwenye mikusanyiko ya ndani ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi’

“Kuzingatia usafi binafsi ikiwemo kunawa mikono kwa maji tirirka na sabuni au kutumia vipukusi(sanitizer)mara kwa mara.

Dk Sichalwe aliongeza kuisisitiza jamii kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya endapo watakuwa na dalili za ugonjwa huo ikiwemo kuendelea kuchukua hatua za kujenga mwili imara kwa kufanya mazoezi na kula vyakula bora, kutoa taarifa za kuwepo watu wenye dalili za ugonjwa huu katika jamii kupitia namba ya simu ya bure 199″alisema Dk. Sichalwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!