Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali kuwatibu wagonjwa damu nchini
Afya

Serikali kuwatibu wagonjwa damu nchini

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema inafanya mkakati wa kuhakikisha watanzania wote wanaougua magonjwa ya damu watibiwe ndani ya nchi kwa kujengea uwezo hospitali zote nchini. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Mganga Mkuu wa serikali Prof. Muhammad Bakari amesema magonjwa hayo ni kama SeliMundu, Upungufu wa damu na Kansa ya damu.

Amesema kuwa lengo la kufanyika kwa mafunzo hayo ni kuhakikisha kunakuwepo na uwezo wa kutibu wagonjwa ndani ya nchi unaimarika.

“Kinachofanyika hapa ni kitu muhimu sana kwetu, kwasababu wataalam wetu wanapata ujuzi mkubwa zaidi kwenye magonjwa ya damu na upatikanaji wa damu na ni heshika kwetu kama nchi kwasababu ni mara ya kwanza yanafanyika nchini kwetu,” amesema.

Aidha Makamu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof Andrea Pembe amesema kuwa kwa idadi ya watoa huduma ya afya Tanzania ni chache ukilinganisha na iddi ya Watanzania wote hivyo nguvu kubwa inahitajika kuongeza watoa huduma katika vituo vya afya.

Amesema kuwa Hospitali za Kanda na Rufaa zina upungufu wa madaktari bingwa na zinahitaji takriban zaidi ya 500 ambapo ni asilimi 79.

“Serikaali kwa ujumla imekuwa ikijitahidi kutoa ufadhiri kwa watu ili waende wakasome lakini kutokana na uwezo wa kusomesha kuwa mdogo hivyo inakuwa ngumu kufanya hivyo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaMakala & Uchambuzi

Uongo, uzushi, tiba ya matende, ngiri maji

Spread the loveKUNA uongo na uzushi katika jamii kuhusu wanaume, wanawake na...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Afya

Kambi ya matibabu ya kibingwa Ruangwa yaacha vilio, DC atoa ombi JAI

Spread the loveMKUU wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma amefunga rasmi kambi...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

error: Content is protected !!