Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Alichokifanya JPM hiki hapa
Habari za Siasa

Alichokifanya JPM hiki hapa

Rais John Magufuli
Spread the love

IFUATAYO ni orodha ya majina ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali walioteuliwa na kuhamishiwa vituo vya kazi leo tarehe 13 Agosti, 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwa niaba ya Rais John Magufuli.

Rais Magufuli amemteua Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, wakati Mhandisi Msafiri Simeon akihamishiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Kwa upande wa wakurugenzi, Rais Magufuli amemhamisha Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Limbe Benard kwenda Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba na kumteua Solomon Kimilike kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba. Vile vile, Ramadhan Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nsimbo.

Mwailwa Smith Pangani amehamishiwa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko akiteuliwa Masumbuko Stephano Magang’hila kuwa mkurugenzi wake. Pia, Upendo Mangali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Kwa mkoa wa Kilimanjaro, Rais Magufuli amemteua Zefrin Kimolo Lubuva kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Mwanga. Wakati Tatu Selemani Kikwete akihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi akitokea Wilaya ya Kibaha.

Mkoa wa Lindi, Rais Magufuli amemhamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwenda Wilaya ya Liwale, wakati Wilaya ya Kilwa akiteuliwa Renatus Blas Mchau kuwa mkurugenzi wake.

Mkoa wa Mara, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Kayombo John amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.Wakati Mkoa wa Mbeya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wakati Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikichukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, James Kasusura. Huku Lucy Mganga akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya ya Kyela.

Mkoa wa Morogoro, Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imechukuliwa na Mhandisi Stephano Kaliwa, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikichukuliwa na Kayombe Lyoba huku Wilaya ya Malinyi akiteuliwa Mussa Mnyeti kuwa mkurugenzi wake. Vile vile, Asajile Mwambambale akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Kanali Emmanuel Mwaigobeko ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara. Kisena Mabuba ameteuliwa  kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, wakati halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe akiteuliwa Ester Chaula kuwa mkurugenzi wake.

Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi iliyoko mkoani Simiyu ameteuliwa Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto, James Mtembelea kuwa mkurugenzi wake. Na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi akiteuliwa Justice Lawrence kuwa mkurugenzi.

Mkoa wa Songwe, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mussa Natty kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Tunduma na Fauzia Hamidu akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe. Na Halmashauri ya Mbozi aliteuliwa Kazimbaya Mkwega kuwa Mkurugenzi.

Mkoani Tabora, Sekiete Yahaya ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Nzega, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge akiteuliwa Martha Daudi Luleka kuwa mkurugenzi.

Mkoa wa Tanga, Rais Magufuli amemteua Nicodemus John Bee kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Koroge, na Gracia Makota akimtuea kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi, huku Halmashauri ya Bumbuli ikichukuliwa na George Haule. Vile vile Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Ikupa Harrison Mwasyoge akiteuliwa kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Lushoto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!