Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba, Yanga zapanguliwa ratiba Ligi Kuu
Michezo

Simba, Yanga zapanguliwa ratiba Ligi Kuu

Spread the love

BODI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania imefanya mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni wiki mbili kabla ya kuanza kwa ligi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema wamelazimika kupangua ligi hiyo kutokana na baadhi ya viwanja vilivyopangwa kufanyika kwa michezo ya ligi hiyo kuwa na shughuli za kijamii.

Mchezo wa ufunguzi kati ya Simba na Tanzania Prison uliopangwa kufanyika 22 Agosti, 2018 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam, umehamishiwa kwenye Uwanja wa Uhuru tarehe hiyo hiyo kutokana na kuwepo na shughuli za kijamii ndani ya uwanja uliopangwa awali.

Aidha mchezo mwengine wa mzunguko wa kwanza wa ligi uliokuwa uwakutanishe Mtibwa Sugar na Yanga katika dimba la Jamhuri Morogoro 23 Agosti, utachezwa kwenye uwanja wa Uhuru na Yanga atakuwa mwenyeji kwenye mchezo huo kutokana na uwanja wa Jamhuri kuwa na shughuli za kijamii mpaka 30 Agosti mwaka huu.

Mabadiliko haya yamekuja kufuatia asilimia 90 za klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara hazimiliki viwanja vyao binafsi bali hutumia viwanja vinavyo milikiwa na serikalai pamoja na Chama Cha Mapinduzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

error: Content is protected !!