January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kupanua shule 100 zipokee wanafunzi wa kidato cha 5, 6

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

 

SERIKALI imepanga wa kuongeza upanuzi wa shule 100 ili ziwe na uwezo wa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Anaripoti Glory Massamu TUDARCo … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 10 Septemba bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde katika kipindi cha maswali na majibu wakati akimjibu) Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Edward Kisau (CCM).

Kisau alihoji, je, ni lini serikali itapandisha shule za sekondari za Lesoit, Dosidosi, Ndedo na Dongo kuwa kidato cha tano na sita kutokana na uhitaji mkubwa wa shule za kidato cha tano na sita Kiteto?

Akijibu swali hilo, Silinde alisema katika shule hizo 100 zitakazopanuliwa, baadhi zitatoka katika wilaya ya Kiteto.

Pia alimuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto kushirikiana na wananchi kujenga mabweni, madarasa na mabwalo kwenye shule za sekondari wilayani hapo ili kuziwezesha kupandishwa hadhi.

Aidha, amesema baadhi ya shule zinashindwa kupandishwa hadhi kutokana na upungufu wa miundombinu ya mabweni, mabwalo na madarasa ya kutosha kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita.

“Serikali inatambua uhitaji mkubwa wa shule za kidato cha tano na sita katika halmashauri ya wilaya ya Kiteto, hata hivyo shule hizo za sekondari zilianzishwa kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji wanaohamahama ili wasome bila kukatisha masomo.hizo ni ya wilaya ya kiteto”, amesema.

error: Content is protected !!