September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Gomez ‘out’ mechi za CAF

Kocha wa Simba, Didier Gomes da Rosa

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa orodha ya makocha ambao hawaruhusiwi kukaa kwenye benchi la ufundi katika mechi za mashindano ya Klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika. Anaripoti Mintanga Hunda TUDARCo … (endelea).

Katika orodha hiyo kocha wa klabu ya Simba, Didier Gomes da Rosa naye atatakiwa kukaa jukwaani kwenye mechi hizo za CAF Champions League.

CAF wanataka kocha mkuu awe na leseni ya UEFA A PRO ambayo ni sawa na leseni A za CAF wakati Didier Gomez da Rosa yeye ana leseni ya UEFA DIPLOMA A.

Vyama vya soka vinavyoongoza vilabu tajwa kwenye orodha (TFF – Tanzania na FERWAFA ya Rwanda) vimeshapewa taarifa mapema.

Didier Gomes da Rosa

Katika orodha hiyo mbali na Dideir Gomes, wengine ni Erradi Mohamed Adil wa APR, Bosa Wasswa wa Express FC, Diego Garzitto wa El Merreikh, Comlan Mathias wa ESAEL FC, Pascal Lafleurial wa DFCB, Roque Sapir wa SD Sagrada Experanca na Ame Khamis wa KMKM.

Taarifa hiyo imezua mjadala kwa wachambuzi wa soka nchini huku wengine wakihoji iwapo uamuzi huo hautaathiri performance ya Simba kwenye mechi zake.

Hata hivyo, kufafanua suala hilo, Kaimu Msemaji wa Klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga alikuwa na haya ya kusema:-

error: Content is protected !!