Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sensa 2022: Majaliwa awapa majukumu wabunge
Habari za Siasa

Sensa 2022: Majaliwa awapa majukumu wabunge

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wabunge wawaelimishe na wawahamasishe wananchi wajitokeza na washiriki katika Sensa ya Watu na Makazi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa na takwimu sahihi kwa makarani wa Sensa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Majaliwa aliyasema hayo jana Jumatatu tarehe 30 Mei 2022, wakati akifungua semina ya wabunge kuhusu Sensa ya Watu na Makazi kwenye ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma.

Alisema kazi ya kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi inapaswa kufanywa na kila mdau wakiwemo Wabunge ambao wajibu wao ni kuwahudumia wananchi.

Majaliwa alisema ni muhimu kwa wabunge kushiriki kikamilifu ili kupata taarifa na takwimu sahihi za idadi ya watu, hali zao za makazi, taarifa za majengo yote nchini hatua ambayo itawawezeshe kuwatumikia vyema wananchi.

“Tunapenda kuona kila Mheshimiwa Mbunge anaona fahari kuwa watu wote katika jimbo lake wamehesabiwa na wametoa taarifa na takwimu sahihi zinazoakisi idadi halisi ya watu na makazi yao katika eneo husika,” alisema

Alisema Tanzania ni moja kati ya nchi chache Barani Afrika ambazo zimeweza kufanya Sensa katika vipindi vyote vya utekelezaji wa Mipango Mikakati ya Umoja wa Mataifa wa Kufanya Sensa.

“Ninapenda kuwaarifu Waheshimiwa Wabunge kuwa maandalizi ya sensa yanaendelea vizuri na sasa tumefikia zaidi ya asilimia 80. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Sensa inafanyika kama ilivyopangwa ikiwa ni pamoja na kutoa matokeo bora kulingana na viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa kwa wakati,” alisema Majaliwa

Akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua semina hiyo, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson aliwashukuru makamisaa na watalaamu wa Sensa kwa semina na mafunzo mbalimbali ambayo wamekuwa wakiwapatia wabunge kwa nyakati na makundi tofauti.

Alisema wabunge wanalichukulia suala la kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika Sensa ya Watu na Makazi na kutoa taarifa sahihi kwa Makarani kuwa ni la msingi.

Dk. Tulia alisema Bunge litatamani kuona kwamba zoezi la sensa na Makazi ya Watu litakalofanyika tarehe 23 Agosti 2022 linaenda vizuri ili takwimu sahihi zitazopatikana ziwasaidie wabunge kuishauri Serikali kupanga na kugharimia shughuli za maendeleo nchini kwa kuzingatia idadi ya watu katika eneo husika.

Kwa upande wake, Kamisaa wa Sensa ambaye pia ni Spika Mstaafu Anne Makinda alisema anashukuru kuona kwamba makundi yote waliyokutana nayo yameonesha nia na dhamira ya kutoa ushirikiano ili kufanikisha Sensa ya Watu na Makazi wakiwemo Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilsihi.

Kauli mbiu ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa ni ‘Sensa kwa Maendeleo Jitokeze Kuhesabiwa’.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!