Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Hukumu ya Sabaya yapigwa kalenda, sababu yatajwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Hukumu ya Sabaya yapigwa kalenda, sababu yatajwa

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha nchini Tanzania imeahirisha kutoa hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita hadi tarehe 10 Juni 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi imeahirishwa leo Jumanne tarehe 31 Mei 2022 kwa sababu Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Dk. Patricia Kisinda kuwa na majukumu mengine nje ya Jiji la Arusha.

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuongoza genge la uhalifu, matumizi mabaya ya madaraka, kujihusisha na vitendo vya rushwa na utakasishaji fedha.

Mbali na Sabaya washitakiwa wengine katika shauri hilo ni, Sylvester Nyengu (26), Enock Togolani (41), Watson Mwahomange (27), John Odemba, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano yakiwamo ya uhujumu uchumi yanayokabili washitakiwa wote.

Ilidaiwa Sabaya akiwa mtumishi wa umma na wenzake, tarehe 20 Januari 2021 Arusha akiongoza genge la uhalifu katika maeneo mbali mbali ya mkoa huu na Kilimanjaro na akiwa Mkuu wa Wilaya, alitumia vibaya madaraka yake akijua wazi ni kosa kisheria.

Mashitaka ya pili dhidi yake Sabaya, ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka jana Arusha akiwa mtumishi wa umma, alishiriki kushawishi rushwa ya Sh milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara wa hapa, Francis Mrosso mkazi wa Kwa Mrombo.

Ilidaiwa kuwa alifanya hivyo ili amsadie katika kesi ya jinai ya ukwepaji kodi, iliyokuwa ikimkabili huku akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, akiwa mtumishi wa umma.

Katika mashitaka ya tatu pia dhidi yake, ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka jana Arusha, aliomba rushwa ya Sh milioni 90 kwa Mrosso ili amsaidie katika kesi hiyo ya kodi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Kwenye mashitaka ya nne ya utakasishaji fedha dhidi ya washitakiwa wote saba, ilidaiwa kuwa Januari 20 mwaka jana Arusha, walipokea Sh milioni 90 za Mrosso na kwenda kuzifanyia matumizi haramu ambayo ni kinyume na sheria.

Hukumu hiyo imeahirishwa ikiwa na kumbukumbu ya ya hivi karibuni Sabaya na wenzake kushinda rufaa katika hukumu nyingine iliyomfunga miaka 30 jela, hivyo adhabu yake kubatilishwa.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilibatilisha hukumu ya miaka 30 jela na kuwaacha huru Sabaya na wenzake wawili, tarehe 6 Mei 2022.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, aliyesikiliza shauri hilo la rufaa namba 129/2021 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Jaji Kisanya alisema baada ya kupitia hoja za pande mbili, Mahakama imejiridhisha kuwapo upungufu wa kisheria kwenye mwenendo wa shauri hilo, hivyo akaamuru kuachwa huru kwa waleta rufaa hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!