Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Biashara SBL yazindua Serengeti Oktoba Festival
BiasharaMichezo

SBL yazindua Serengeti Oktoba Festival

Spread the love

 

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Lite imezindua Tamasha kubwa la Serengeti Oktoba Festival litakalofanyika tarehe 21 Oktoba, 2023 katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi huyo, Meneja wa Bia ya Serengeti Lite, Ester Raphael amesema tamasha hilo ambalo litakuwa kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo litafanyika katika nchi nne za Tanzania, Kenya, Uganda na Sudan Kusini.

Ester amesema katika tamasha hilo kutakuwa na burudani za kutosha ikiwa vinywaji lakini pia itatoa fulsa kujua tamaduni kutoka katika nchi hizo za Afrika Mashariki na Kati.

“Wengi wana amini matamasha kama hayo yanakuwa na unywaji wa bia zaidi lakini Serengeti tumeamua kuja tofauti kwa kuonyesha tamaduni tofauti kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

“Pia tutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa kutoka katika nchi hizo ikiwa pamoja na aina za vyakula kutoka katika nchi washiriki,” alisema Ester.

Naye Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries Limited, Rispa Hatibu amesema tamasha hilo itafanyika kwa mara ya kwanza nchini lakini pia litaenda katika nchi za Kenya, Uganda na Sudan Kusini.

Anitha Rwehumbiza, Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi wa Serengeti Breweries Ltd, amesema pamoja na tamasha hilo kuwa sehemu ya burudani na kujua tamadauni za nchi shiriki, lakini watarudisha fadhira kwa jamii kwa kutoa ajira kwa watoa huduma watakaokuwepo katika tamasha hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Pesa ipo huku Meridianbet, beti sasa

Spread the love  WIKIENDI inaishia leo hii jaman kama bado hujasuka mkeka...

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Mwenge

Spread the love  KAMPUNI ya Meridianbet imefika maeneo ya Mwenge jijini Dar-es-salaam...

Biashara

Serengeti yakabidhi mkwanja kwa mshindi wa Maokoto ndani ya Kizibo

Spread the love Mshindi wa Maokoto ndani ya kizibo kutoka Kahama Mjini...

Biashara

Ushindi rahisi unpatikana kila ukicheza kasino ya Hot Joker

Spread the love  HOT Joker Fruits 20 ni mchezo wa sloti ya...

error: Content is protected !!