Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Biashara Waziri Mkuu aiagiza PURA kuharakisha zoezi la kunadi vitalu
BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri Mkuu aiagiza PURA kuharakisha zoezi la kunadi vitalu

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuharakisha mchakato wa kunadi vitalu vya mafuta na gesi asilia nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 20 Septemba 2023 alipotembelea banda la PURA kwenye kongamano la nishati linaloendelea kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni kuhusu kuharakisha mchakato wa kunadi vitalu vya utafutaji mafuta na gesi asilia nchini. Ametoa maelekezo hayo Septemba 20, 2023 kwenye kongamano la nishati linaloendelea katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mnaongeza kasi katika mchakato wa kunadi vitalu vyetu ili wawekezaji waje kuwekeza katika utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini ili nchi inufaike,” aliongeza.

Akitoa taarifa fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni alieleza kuwa mamlaka inaendelea na shughuli za awali za utekelezaji wa duru ya tano ya kunadi vitalu vya mafuta na gesi kwa maeneo ya nchi kavu na baharini kwa lengo la kuongeza wawekezaji.

Mjiofizikia wa PURA Josephine Jumanne akitoa maelezo kuhusu zoezi la kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa washiriki wa kongamano la nishati waliotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa sambamba na maandalizi hayo PURA inaendelea kuweka mipaka ya vitalu vitakavyonadiwa na kuandaa vifurushi vya data (Data Packages) kwa kila kitalu.

“Hadi sasa vitalu 26 vinafanyiwa uchambuzi ili kupendelezwa kwa ajili ya kuingizwa katika mnada. Kati ya hivyo, vitalu 15 vipo nchi kavu na 11 vinapatikana baharini,” alifafanua Mhandisi Sangweni alibainisha kuwa Serikali inatarajia kuzindua zoezi la kunadi vitalu kati ya mwezi Desemba, 2023 hadi Machi, 2024 baada ya kukamilika kwa shughuli za maandalizi zinazoendelea.

Inaelezwa kuwa zoezi la kunadi vitalu linakadiriwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 3.5. Aidha, kwa mwaka 2023/24 Serikali kupitia PURA imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kazi za awali za maandalizi ya zoezi hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Biashara

Cheza sloti ya Zombie Apocalypse na ushinde kirahisi

Spread the love Wengi wetu hupenda filamu za Mazombie huwa zinatishakidogo lakini...

Biashara

Ushirikishwaji wa wafanyakazi ni muhimu katika utekelezaji wa sera za afya na usalama kazini

Spread the love  KILA ifikapo Aprili 28 ya kila mwaka, dunia huadhimisha...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

error: Content is protected !!