Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia kuongoza vikao vya CCM Dodoma
Habari za Siasa

Samia kuongoza vikao vya CCM Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, kinatarajia kufanya vikao vyake vya kawaida jijini Dodoma, kuanzia tarehe 15 hadi 18 Desemba 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa kwa umma leo Jumanne, tarehe 14 Desemba 2021 na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka.

Taarifa ya Shaka imesema kuwa, kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kitafanyika tarehe 18 Desemba mwaka huu, kikitanguliwa na vikao vya Kamati Kuu na Sekretarieti ya halmashauri hiyo.

“Halmashauri Kuu ya CCM itakutana Desemba 18, 2021 chini ya Mwenyekiti wetu, Rais Samia. Kikao hicho kitatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu ya Halmashauri ya CCM Taifa na Sekretarieti ya Halmashauru Kuu ya CCM Taifa kuanzia Desemba 15, 2021,” imesema taarifa ya Shaka.

Taarifa hiyo imesema kuwa, vikao hivyo ni vya kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya 1977 Ibara ya 108.

“Vikao vyote ni vya kawaida ambavyo vitafanyika makao makuu ya CCM jijini Dodoma, ambaoo maandalizi ya vikao hivyo yamekamilika,” imesema taarifa ya Shaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!