May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Karagwe, Misenyi kinara usafi wa mazingira

Spread the love

 

IMEELEZWA kuwa Wilaya za Karagwe na Misenyi zilizopo mkoani Kagera ni kati ya wilaya ambazo zimefanya vizuri katika usafi wa mazingira. Anaripoti Danson Kaijage, Kgera … (endelea).

Aidha, wilaya ya Kyerwa iliyopo katika mkoa huo imetajwa kutofanya vizuri katika suala la utunzaji wa mazingira.

Hayo yameelezwa na Afisa Afya Mkoa wa Kagera, Zabron Seguru alipokuwa akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa mkoa juu ya Afya ya Mazingira na usafi katika mkutano wa mkuu wa mwaka wa Afya, Mazingira na Usafi wa mwaka 2021.

Akiwasilisha taarifa hiyo amesema kuwa Mkoa wa Kagera ni Mkoa ambao unapakana na nchi zaidi ya mbili huku ukiwa na wilaya 8 , kata 192 na visiwa 25.

Amesema Kagera imepokea Sh milioni 2.7 ambazo zimewezesha kutengeneza miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza usafi wa mazingira.

“Pesa hizo zimewezesha utengenezaji wa miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwezesha ujenzi wa vyoo bora katika maeneo mbalimbali pamoja na kuwezesha usalama wa usafi katika vituo 70.

“Katika kuhakikisha usafi wa mazingira unazingatiwa na unapewa kipaumbele pamekuwa pakiandaliwa mashindano mbalimbali jambo ambalo limeonesha wazi kuwa wilaya ya Karagwe na Misenyi zikionekana kufanya vizuri zaidi” amesema Segeru.

Kwa upande afisa Afya Mkoa wa Dodoma, Paul Mageni amesema kwa Mkoa wa Dodoma umefanya vizuri katika suala zima la usafi na mazingira.

Mageni amesema kwa sasa Mkoa wa Dodoma umeongeza idadi ya vyoo bora katika maeneo mbalimbali ikiwa ndani ya Jiji pamoja na wilaya zake.

“Mfano katika wilaya ya Mpwapwa wamekuwa wakifanya vizuri zaidi katika usafi wa mazingira kutokana na uboreshwaji wa mazingira” ameeleza Mageni.

error: Content is protected !!