Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Samia ashtushwa kifo cha Jessie
Kimataifa

Samia ashtushwa kifo cha Jessie

Komred Yasmin 'Jessie' Duarte
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa masikitiko kicho cha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha African National Congress (ANC), Komred Yasmin ‘Jessie’ Duarte aliyefariki mwishoni mwa wiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ameelezea masikitiko yake hayo kupitia taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Julai, 2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.

Rais Samia ameelekeza salamu zake za rambirambi kwa Mwenyekiti wa African National Congress (ANC) Komredi Gwede Mantashe na Rais wa Afrika Kusini Komred Cyril Ramaphosa.

Amesema Marehemu Yasmin alikuwa mmoja wa viongozi imara wa ANC tangu enzi za mapambano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo, akisimamia misingi ya utu kwa ajili ya jamii yenye usawa bila kijali rangi, jinsia wala utaifa ndani ya Afrika Kusini, Afrika na Dunia kwa ujumla kupitia nafasi mbalimbali alizoshika.

“Nimepokea taarifa za msiba huu kwa masikitiko makubwa. Salamu za rambirambi katika wakati huu mgumu ziwafikie familia yake, ndugu jamaa na marafiki.

Tuko pamoja na makomredi wote wa ANC, Afrika Kusini kwa ujumla na kwingineko kote ambao mbali na maisha ya kikazi ya Komredi Jessie pia walishirikiana naye kwa namna moja au nyingine kutekeleza wajibu wa kizalendo wa kupigania na kulinda uhuru wa Mwafrika na nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali,” amesema.

Rais Samia alisema kitendo cha Komredi Jessie kuaminiwa kuwa msaidizi maalum wa Hayati Nelson Mandela na kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ANC tangu mwaka 2002 na kuwa Naibu Katibu Mkuu kuanzia 2012 kinadhihirisha uwezo wake.

Amesema Marehemu Jessie amekuwa sehemu ya mafanikio kwa chama hicho tangu zama za kupigania ukombozi Serikali ya ANC na Afrika Kusini kwa ajili ya jamii yanye ustawi wa haki, usawa na maendeleo ya watu wa nchi hiyo na Afrika kwa ujumla.

Mwisho

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!