August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinyi aipa JKU kazi alizowatimua wakandarasi binafsi

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amesema ameridhishwa na kazi zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na kuahidi kutoa kazi nytingi zaidi kwa jeshi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Mtindo huo wa Dk. Mwinyi ulitumiwa pia na Rais wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli wakati akiwa madarakani ambapo ilishuhudiwa zabuni nyingi za ujenzi likiwepewa Shirika la Suma-JKT linalomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Akizungumza leo katika uzinduzi wa majengo ya wafanyabiashara wa mbao visiwani humo, Dk. Mwinyi amesema kampuni nyingi binafsi zimeonesha kushindwa kufanya kazi huku JKU ikifanya vizuri.

Dk. Mwinyi ametaja kushindwa kwa kampuni binafsi katika ujenzi wa masoko matatu pamoja na shule ambapo jana alimsimamisha mkandarasi Kampuni ya Ujenzi ya Associated Investment Service Ltd ya Dar es Salaam kufanya kazi Zanzibar kwa kile alichodai haina uwezo.

Pia, alisitisha mkataba wa mkandarasi huyo wa ujenzi wa Shule ya Mtopepo katika Shehia ya Monduli Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini.

Rais Mwinyi alichukua hatua hiyo, baada ya kutembelea ujenzi wa shule hiyo yenye ghorofa tatu. Kwa mujibu wa mkataba huo ulioanza Februari mwaka huu, ujenzi unatakiwa kukamilika Agosti mwaka huu, lakini bado upo asilimia 35.

“Hivi karibuni kuna masoko tuliwapa watu hili la Kwerekwe, Jumbi na Chuini lakini kwa bahati mbaya hawakufanya vizuri baada ya kuwapa maana ilikuw ani sekta binafsi kwahivyo tumetolea maamuzi kwamba Serikali itabeba kazi hiyo ya kuyajenga yale masoko tuwape watu maeneo mazuri ya kufanyia kazi,” amesema Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi amesema kazi za ujenzi wa masoko hayo sasa zitatolewa kwa JKU.

“Napenda kuwapongeza kwa dhati jeshi la Kujenga Uchumi kwa kazi mnayoifanya, kwakweli lazima nikiri kwamba nimeridhika, tumekupeni kazi nyingi na kila ninapokwenda mmefanya kwa ufanisi na kwa wakati, hongereni sana.

Sasa tuna viporo vyetu jana tumemnyang’anya mtu skuli sehemu huko lazima tuwape JKU, lakini tuna masoko wale watu tuliowapa masoko yetu matatu wakashindwa lazima tuwape vikosi masoko yale.

Nataka nikuambieni kitu kimoja kwa kazi hii mmeonesha mnaweza na mimi nitakupeni kazi nyingi sasa msije mkaniangusha mbele ya safari, nina uhakika mtafanya kwasababu ninyi mna nidhamu ya kijeshi,” amesema Dk. Mwinyi.

Dk. Mwinyi amewataka mufanya kazi vizuri na vijana wote watakaoshiriki katika miradi hiyo kwa kujitolea orodha yao uwekwe vizuri, “kuna jambo nataka kufanya.”

error: Content is protected !!