Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia amtumbua mkurugenzi Dart
Habari MchanganyikoTangulizi

Samia amtumbua mkurugenzi Dart

Spread the love

Hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan  ametengua uteuzi wa Dk. Edwin P. Mhede aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).


Dk. Mhede ambaye imeelezwa atapangiwa kazi nyingine, nafasi yake imechukuliwa na Dk. Athuman Kihamia aliyewahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha.

Hatua hiyo inajiri baada ya kuzorota kwa muda mrefu kwa huduma za usafiri wa mabasi hayo jijini Dar es Salaam na kuzidisha adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hilo huku uongozi wa  Dart ukiendelea kukaa kimya bila kuchukua hatua zozote.

Aidha, taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus pia Rais Samia amemteua Musa N. Kuji kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Kuji alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!