Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Corona yaua 10,000 sikukuu za Krismasi, mwaka mpya
AfyaKimataifa

Corona yaua 10,000 sikukuu za Krismasi, mwaka mpya

Spread the love

Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema mikusanyiko ya sikukuu za mwisho wa mwaka imesababisha kasi ya kusambaa kwa virusi vya COVID-19 dunia vilivyosababisha vifo vya watu 10,000 Disemba mwaka jana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Ghebreyesus alisema karibu vifo 10,000 viliripotiwa mwezi Disemba, wakati watu waliolazwa hospitali katika mwezi huo waliongezeka kwa asilimia 42 katika nchi takribani 50, hasa za Ulaya na Marekani ambazo zilishirikiana taarifa kama hizo.

Ijapokuwa vifo 10,000 kwa mwezi ni kidogo sana kuliko wakati janga hili lilipoanza, kiwango hiki cha vifo vinavyoweza kuzuilika hakikubaliki,” alisema mkurugenzi huyo wa WHO alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva nchini Uswis.

Alisema ni uhakika kwamba visa vinaongezeka katika maeneo mengine ambayo hayajaripoti.

Pia ametoa wito kwa serikali kuendelea kufuatilia na kutoa fursa ya kuendelea kupata matibabu na chanjo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

error: Content is protected !!