July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sabaya bado anakinga mshahara

Lengai ole Sabaya

Spread the love

 

WAKATI mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, akifikishwa mahakamani na kutupwa katika mahabusu ya gereza la Kisongo, mkoani Arusha, taarifa zinasema, “mtuhumiwa huyo” bado analipwa mshahara na serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ambazo Raia Mwema imezipata zinasema, hatua ya Sabaya kuendelea kulipwa mshahara, inatokan na utekelezaji wa sheria ya utumishi wa umma, ambayo inatoa haki kwa mtumishi aliyesimamishwa kazi, kulipwa mshahara wake.

Aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Hai na Hayati Rais John Pombe Magufuli, tarehe 18 Julai mwaka 2018 na kusimamishwa kazi, 13 Mei 2021 na Rais Samia Samia Suluhu Hassan, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Undani wa habari hii, kujua Waziri wa utumishi wa umma, Mohamed Mchengerwa, kaeleza nini kuhusu kinachoendelea na jinsi Sabaya alivyoingia kwenye utumishi, Soma Gazeti la Raia Mwema, la leo Jumamosi, tarehe 12 Juni 2021.

error: Content is protected !!