Saturday , 10 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Askari 34,106 wapandishwa vyeo Tanzania
Habari Mchanganyiko

Askari 34,106 wapandishwa vyeo Tanzania

Spread the love

 

WIZARA Mambo ya Ndani ya Tanzania, imewapandisha vyeo maafisa, wakaguzi na askari wa ngazi mbalimbali 34,106 waliostahili kupandishwa vyeo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019/2020 na 2020/2021. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, 11 Juni 2021 na Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu Jijini Dodoma.

Amesema jeshi la polisi limewapandisha vyeo jumla ya maafisa, wakaguzi na askari 26,464 kati ya idadi hiyo jumla ya warakibu waandamizi wa polisi 110 wamepandishwa cheo kuwa makamishna waandamizi.

“Warakibu wa Polisi 110 wamepandishwa cheo na kuwa warakibu waandamizi wa polisi, warakibu wa polisi 241 wamepandishwa cheo na kuwa warakibu wa polisi.”

“Wakaguzi wa polisi 745 wamepandishwa cheo na kuwa Warakibu wasaidizi wa polisi, wakaguzi wasaidizi 890 wamepandishwa Cheo na kuwa Wakaguzi wa polisi na jumla ya askari R&F 4,148 wamepandishwa vyeo na kuwa Wakaguzi wasaidizi wa polisi,” amesema Simbachawene

“Askari wa R&F 20,220 wamepandishwa vyeo mbalimbali, kutoka polisi Koñstebo kwenda Koplo ni 13,751, kutoka koplo kwenda Sajini 5,619, kutoka Sajini kwenda Stafu Sajini ni 800 na kutoka Sajini kwenda Sajini Meja ni askari 50,” amesema

Simbachawene pia amesema, kwa upande wa Jeshi la Magereza limewapandisha vyeo jumla ya maafisa, wakaguzi na Askari 6,310 kati ya idadi hiyo,jumla ya Warakibu waandamizi wa Magereza 7 wamepandishwa cheo na kuwa makamishna wasaidizi wa Magereza,Warakibu wa Magereza 14 wamepandishwa cheo na kuwa warakibu waandamizi wa Magereza.

Aidha Simbachawene amesema, warakibu wasaidizi wa Magereza 102 wamepandishwa cheo na kuwa warakibu wa Magereza, wakaguzi wa Magereza 75 wamepandishwa cheo na Warakibu wasaidizi wa Magereza,Wakaguzi wasaidizi wa Magereza 69 wamepandishwa cheo na kuwa Wakaguzi wa Magereza.

Katika ufafanuzi, Simbachawene amesema, jumla ya askari Magereza 938 wenye ngazi ya R& F wamepandishwa vyeo na kuwa Wakaguzi wasaidizi wa Magereza.

Amesema, askari wa R&F 5,105 wamepandishwa vyeo mbalimbali kutoka Wadres kwenda Koplo ni 2,632, kutoka Koplo kwenda Sajini 1,340, kutoka Sajini kwenda Stafu Sajini ni 1,103 na kutoka Stafu Sajini kwenda Sajini Meja ni 30.

Akizungumzia Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, Simbachawene amesema, Jeshi hilo limepandisha vyeo jumla ya Maafisa, Wakaguzi na askari 149, kati ya idadi hiyo jumla ya Wakaguzi wasaidizi wa Zimamoto na Uokoaji wanne, wamepandishwa cheo na kuwa Wakaguzi wa Zimamoto na Uokoaji.

Aidha askari wa F&F 145, wamepandishwa cheo kutoka Koplo kwenda Sajini.

Waziri huyo pia amesema, kwa upande wake Idara ya Jeshi la Uhamiaji, limepandisha vyeo jumla ya maafisa, wakaguzi na askari 1,183, kati ya idadi hiyo Jumla ya Warakibu waandamizi wa uhamiaji 9 wamepandishwa Cheo na kuwa Makamishna Wasaidizi wa Uhamiaji.

“Warakibu wasaidizi wa Uhamiaji 49 wamepandishwa cheo na kuwa Warakibu wa Uhamiaji,Wakaguzi wa Uhamiaji 65 wamepandishwa cheo na kuwa warakibu Wasaidizi wa Uhamiaji,Wakaguzi wasaidizi wa Uhamiaji 421 wamepandishwa cheo na kuwa Wakaguzi wa Uhamiaji.”

“Jumla ya askari wa Uhamiaji 407 wenye ngazi ya R&F wamepandishwa Cheo na Kuwa Wakaguzi wa Uhamiaji,” amesema

“Askari wa R&F 232 wamepandishwa vyeo mbalimbali, kutoka Konstebo kwenda Koplo wa Uhamiaji ni 31, kutoka Konstebo kwenda Sajini ni 2 kutoka Koplo kwenda Sajini ni 139,kutoka Sajini kwenda Stafu Sajini ni 59 na kutoka Sajini kwenda Meja Sajini ni mmoja” ameeleza Simbachawene.

Aidha Simbachawene amesema, wote waliopandishwa vyeo wataanza kupatiwa mafunzo kwa awamu.

“Wote waliopandishwa vyeo wataanza kupatiwa mafunzo mbalimbali kwa awamu kati ya miaezi sita na mitatu na tayari Rais Samia Suluhu Hasani ameisha Toa fedha za mafunzo hayo” amesema Simbachawene

Hata hivyo, Simbachawene hakuweza kutaja kiwango cha fedha zitakazotumika kuendesha mafunzo ambayo ya askari hao watakaopandishwa vyeo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!