Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rwanda yaadhimisha miaka 29 ya mauaji ya Kimbari
Kimataifa

Rwanda yaadhimisha miaka 29 ya mauaji ya Kimbari

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Spread the love

 

WANANCHI wa Rwanda leo Ijumaa, tarehe 7 Aprili 2023, wanaadhimisha miaka 29 ya mauaji ya Kimbari, ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua watu karibu milioni moja wengi wao wakiwa ni Watutsi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Rwanda … (endelea).

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100, viliteketeza maisha ya mamilioni ya wananchi wa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Vilijiri siku moja tu baada ya kudunguliwa kwa ndege iliyombeba aliyekuwa rais wa wakati huo, Juvénal Habyarimana pamoja na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira.

Viongozi hao wawili walikuwa wametokea kwenye mkutano wa kilele nchini Tanzania ambako walikuwa wanajadili mzozo huo wa Rwanda.

Mauji ya Kimbari ya mwaka 1994, ni miongoni mwa matukio mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Rwanda.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, bila uthibitisho, amekuwa akiyalaumu mataifa makubwa kukalia kimya wakati nchi yake ilipokuwa ikipitia jinamizi la mauaji hayo.

Siku ya tarehe 7 Aprili ya kila mwaka, kuanzia asubuhi wananchi kuanzia ngazi ya kijiji wanakusanyika pamoja ambapo wanasikiliza historia ya jinsi mauaji hayo yalivyotokea, sababu yake na namna taifa lilivyojikwamua hadi hapa lilipo.

Hata hivyo, katika mihadhara iliyotolewa leo kote nchini, baadhi ya wananchi wameonyesha wasiwasi kwamba wakati Rwanda ikikumbuka mauaji haya, kwa upande mwingine mitandao ya kijamii kutoka ndani na nje ya taifa hilo, inaingia kwenye mrengo uleule wa vyombo vya habari vilivyochochea na kueneza ya mauaji.

Akizungumza katika maadhimisho haya, Rais Kagame, amesema kuwa wao ni nchi ndogo, lakini ni wakumbwa mno kwenye haki, na baadhi ya hao mnaowasikia ni nchi kubwa na zenye nguvu lakini ni wadogo sana katika suala la haki.

Aliongeza, “hawana mamlaka ya kutoa mafunzo kwa mtu yeyote kwa sababu wao ni sehemu ya historia hii ambapo zaidi ya watu wetu milioni waliangamizwa.”

Amesema, wananchi sasa wameweza kupiga hatua ya maendeleo kutokana na sera inayoendelea kufanikiwa ya umoja na maridhiano ambayo kimsingi haikuwa rahisi kufikiwa.

“Hebu wewe fikiria baadhi yetu sisi tuliokuwa na silaha, kama tungejiruhusu kuwaendea wale waliokuwa wakifanya mauaji ya watu wetu na kuwaua kiholela kama ambavyo walikuwa wakiwaua ndugu zetu. Kwanza, tungelikuwa na haki ya kufanya hivyo…lakini hatukuchukua hatua hiyo tuliwaacha,” alieleza.

Hata hivyo, wakati kiongozi huyo akijitapa kuwa mlinzi wa haki za kiraia na mtetezi mkuu wa demokrasia, Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linamtuhu Kagame kukandamiza wapinzani na wachambuzi nchini mwake, kutokana na tofauti za kimtazamo.

Katika ripoti yake iliyochapishwa juzi Jumatano, Human Rights Watch inasema, imechunguza mashtaka na maamuzi ya majaji dhidi ya raia kadhaa wa Rwanda ambao wamekuwa wakitoa maoni ya kuikosoa serikali.

Mkuu wa Human Rights Watch katika kanda ya Afrika ya Kati, Lewis Mudge, amesema ni vigumu sana kwa watu nchini Rwanda, kutoa maoni yanayoikosoa serikali.

Alisema: ”Mfano mmoja, ni ule wa Kizito Mihigo, aliyekamatwa na kutupwa jela bada ya kuimba wimbo ambao walionyesha mshikamano na wahanga wa uhalifu wowote, nchini Rwanda wimbo huo ulichukuliwa kama mstari mwekundu.”

Baadaye polisi walisema, Kizito alijinyonga akiwa rumande; shirika limemnukuu Dieudonne Niyonsenga (Cyuma Hassan), ambaye amefuguliwa mashtaka mahakamani, baada ya kuzungumzia visa vya haki za binadamu na ufisadi nchini humo na mwaka uliopita, alihukumiwa jela miaka saba.

Aidha, shirika hilo limesema, kumekuwepo na sheria ambazo zinaminya uhuru wa kujieleza katika taifa hilo, hasa kwa wanasiasa na wachambuzi wanaotoa maoni yao kupitia mitandao ya kijamii.

Shirika limesema, limefanikiwa kuwahoji baadhi ya wanahabari walioshtakiwa pamoja na wanasiasa 11 wa upinzani waliokamatwa kwa kutoa mitazamo yao.

Naye Lewis Mudje amesema, uhuru wa majaji nchini Rwanda upo mashakani na nilazima baadhi ya sheria nchini humo zirekebishwe.

”Kwetu sisi viongozi wa kishiria nchini Rwanda hawana uhuru wa kuhakikisha haki ya kutoa maoni imeheshimiwa kulingana na sheria ya kimataifa. Tumeshuhudia watu wanaohukumiwa kwa sababu ya kutoa maoni yao. Watu hao wanatakiwa kuachiwa huru haraka na bila masharti yoyotem,” alieleza.

Machi 3 mwaka jana, Human Rights Watch imesema ilimwandikia barua Waziri wa Sheria Emmanuel Ugirashebuja ili kutoa maoni kuhusu uchunguzi wake na kuomba taarifa kuhusu hatua za mamlaka ya Rwanda kushughulikia ukiukaji wa haki ya uhuru wa kujieleza. Lakini Serikali haijajibu.

Shirika limetaka jumuiya ya kimataifa kuchukua msimamo na kushinikiza mamlaka kusitisha unyanyasaji, na kufuta mashitaka yote yanayowakabili wanachama wa upinzani, watumiaji wa YouTube na waandishi wa habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!