Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Afrika Ruto, Mudavadi waungana uchaguzi mkuu Kenya
AfrikaKimataifa

Ruto, Mudavadi waungana uchaguzi mkuu Kenya

Spread the love

Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amethibitisha rasmi kuwa chama kipya cha UDA kitaingia katika ushirikiano na chama cha Musalia Mudavadi – cha Amani National Congress (ANC) na chama cha FORD-Kenya kinachoongozwa na Moses Wetangula. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akiwahutubia wajumbe wa chama cha ANC katika ukumbi wa Bomas of Kenya mwishoni mwa wiki, Ruto amefichua kwamba alifanya majadiliano ya muda mrefu yenye mafanikio, yaliyolenga kuunda muundo wa kisiasa, na wawili hao.

Amesema muungano wao mpya utafanya mikutano mingi nchini humo kuanzia wiki ijayo na kuwa wataanza safari yao mpya ya kisiasa Jumatano mjini Nakuru kabla ya kuelekea Magharibi mwa Kenya siku ya Ijumaa na Kenya ya Kati wikendi ijayo.

“Tumekuwa na mazungumzo na ndugu zangu na kukubaliana kwamba Kenya ni kubwa kuliko sisi sote, tunakwenda kujitoa mhanga. Tumeanzia Bomas na kituo chetu kingine kitakuwa Nakuru.” Ruto alisema.

Kuingia kwa Ruto katika muungano huo hata hivyo ni kubatilisha msimamo wake mkali wa awali kuhusu ushirikiano wa kisiasa kabla ya uchaguzi ambapo amesisitiza mara nyingi kwamba hakuwa tayari kushirikiana na vyama ambavyo alivitaja kuwa vidogo na vya kikabila.

Kiongozi huyo kwa muda mrefu amekuwa akiwashinda viongozi wanaotaka kuungana naye kuvunja vyama vyao na kujiunga na vazi lake la UDA.

Hata hivyo, Vinara wa Muungano wa One Kenya Alliance (OKA) Gideon Moi wa chama cha KANU na mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka waliondoka katika hafla hiyo baada ya William Ruto kuwasili katika ukumbi huo kuhudhuria hafla hiyo ambayo Mudavadi alisema kuwa itatetemesha siasa za taifa hilo.

Wawili hao hawakuelezea sababu ya kuondoka kwao lakini inashukiwa kuwa kisa cha kuhisi kusalitiwa kwa sababu wao pia wanawinda kiti cha urais katika uchaguzi mkuu Agosti 9, 2022.

Kinara mwingine wa OKA, Moses Wetangula wa chama cha Ford Kenya hata hivyo alisalia katika ukumbi huo akikaa mkabala na Ruto.

Ruto aliwasili katika ukumbi huo mchana wa jana tarehe 23 Januari 2022, muda mfupi tu baada ya kufahamika kuwa alikuwa amealikuwa amealikuwa katika mkutano huo.

1 Comment

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. … MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA… MHE. KULE ULIKOOA KUNA JAMBO LETU LA KATIBA MPYA

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!