Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Majaliwa atoa ujumbe kwa vijana, halmashauri
Habari za Siasa

Majaliwa atoa ujumbe kwa vijana, halmashauri

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa Kitanzania wahakikishe wanajiwekea malengo ya kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia Taifa kupata maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Pia, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Ameyasema hayo leo Jumatatu, tarehe 24 Januari 2022, alipokagua ujenzi wa madarasa ya shule za Sekondari za Gehandu na Nowu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Majaliwa amesem Serikali kwa upande wake imejipanga ipasavyo na itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia ili kuwawezesha kufikia malengo yao.

Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19. “Vijana someni kwa bidii hadi mfike chuo kikuu.”

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote ziweke mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato yao ya ndani ili wanafunzi wakae shuleni na kupata muda wa kutosha wa kujisomea.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuwatumikia Watanzania na kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM.

Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Gehandu, Mwalimu Gadiel Bei alimshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa.

Alisema mbali na madarasa hayo pia wamejenga madarasa mengine matano kati yake mawili yametokana na fedha za ruzuku ya EP4R na matatu ni nguvu za wananchi na Halmashauri.

Mwalimu Bei alisema kukamilika kwa madarasa hayo kutaiwezesha shule hiyo yenye wanafunzi 945 wa kidato cha kwanza hadi cha sita kuongeza tahasusi nyingine ya kidato cha tano kuanzia mwezi Julai 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!