Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Rais Mwinyi mgeni rasmi mkutano wa bima Z’bar
Habari Mchanganyiko

Rais Mwinyi mgeni rasmi mkutano wa bima Z’bar

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi atahutubia mkutano mkubwa wa wadau wa bima kutoka ndani na nje ya nchi, wenye lengo la kujadilia masuala mbalimbali yahusuyo bima ikiwemo afya na kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mwinyi atahutubia siku ya kwanza kati ya tatu ya mkutano huo utakaoanza keshokutwa hadi Ijumaa, visiwani Zanzibar umeandaliwa na Chuo cha Africa College of Insurance & Social Protection (ACISP) cha jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, tarehe 24 Januari 2022, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa chou hicho, David Sawe amesema, katika kipindi hicho cha mkutano, watabadilishana mawazo na kufanya tahimini wapi wametoka, walipo na wanakwenda wapi.

Amesema, hoja kuu zitakazoangaliwa ni “bima ya afya na jinsi kampuni binafsi zinazoweza kusaidia huduma za bima kwa wote; bima ya maisha ambayo iko chini kuliko inavyotakiwa kwa nchi zetu za Afrika, tunapaswa kuiongeza.”

Mwenyekiti huyo amesema, hoja nyingine ni bima ya kilimo ambayo imezungumzwa sana hivyo kutokana na changamoto zake, wadau wa bima wanapaswa kuungana kuona kipi kinaweza kufanyika na mwisho kukuza uwezo wa watumishi kwenye kampuni za bima.

“Ni kipindi ambacho watu wanakaa na kutafakari kuhusu mwenendo, mafanikio na changamoto zilizopo mbele yetu ili kukuza biashara ya bima kwani hili ni suala nyeti ambalo wadau watalijadili,” amesema.

“Tunapenda kuwajulisha kwamba, mkutano wetu huu utafunguliwa na Rais Hussein Ali Mwinyi. Atatoa hotuba ya ufunguzi na kutakuwa na viongozi wa juu kutoka Afrika na makamisha mbalimbali wa bima,” amesema Sawe

Naye kaimu mkurugenzi wa mipango, tafiti na maendeleo ya masoko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Zakaria Muyengi amesema suala la bima ni hitaji muhimu kwa wananchi.

Amesema na Serikali imeandaa mkakati wa kuendeleza sekta ya fedha utakaochukua miaka kumi, “kwa hiyo tunautekeleza na tunapokwenda kwenye huu mkutano, tunakwenda kutekeleza mpango mkakati wa mapinduzi bima.”

“Kwa sasa majanga yameongezeka, ni lazima Watanzania wote waweze kutumia bima na sisi TIRA tuko tayari na mkutano huu wa Zanzibar na wadau wote wawepo,” amesema.

Muyengi amesema, kwa sasa uelewa wa wananchi kuhusu bima ni asilimia 36, “na malengo ni kufikia asilimia 80 mwaka 2030.”

Kwa upande wake, Martin Masawe, Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB ambao ni miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo amesema, “sisi kama NMB tuna nafasi kubwa ya kukuza soko la bima nchini kwa kukuza uelewa kwa wananchi.”

“Hii inatokana na ukubwa wa benki hiyo na kwa matawi yetu yaliyosambaa nchi nzima, tunayaweza kuyatumia ili kuwafikia wananchi na kueleza kwa kina undani na umuhimu wa bima,” amesema Masawe

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi vifaa tiba hospitali Mtwara  

Spread the loveBENKI ya NMB Kanda ya Kusini imetoa msaada wa vifaa...

Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Spread the love  MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!