RIPOTI kuu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, imewasilishwa bungeni jijini Dodoma, kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Ripoti hiyo imewasilishwa leo tarehe 15 Aprili 2024, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande, ikiwa ni wiki mbili baada ya CAG Charles Kichere, kuikabidhi kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, tarehe 28 Machi mwaka huu.
Akiwasilisha hati ya ripoti hiyo mezani, Chande amesema imebeba ripoti 21 za ukaguzi, ikiwemo ripoti ya CAG kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha za Serikali kuu, ripoti kuhusu ukaguzi wa taarifa za fedha za mamlaka za serikali za mitaa, ripoti ya ukaguzi wa taarifa za fedha za miradi ya kimkakati na ripoti ya ukaguzi wa mashirika ya umma.
Ripoti nyingine ni ya ukaguzi wa ufanisi na ripoti ya ukaguzi wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Leave a comment