Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Biashara TPA yakamilisha mifumo ya TEHAMA, ikiwa ni utekekezaji wa maagizo ya Rais Samia
Biashara

TPA yakamilisha mifumo ya TEHAMA, ikiwa ni utekekezaji wa maagizo ya Rais Samia

Spread the love

 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), chini ya Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa imefanikiwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kuwa na mifumo Madhubuti ya Tehama inafanya kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salam … (endelea).

Katika mwaka wa fedha 2022/2023 miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ikiwa pia ni Pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Rais ni kama ifuatavyo;

  • Kukamilika kwa asilimia kubwa mradi wa TEHAMA (Enterprise Resource Planning, ERP) ambao hutumika katika kuandaa na kuhifadhi taarifa za kifedha na kuunganisha shughuli za Idara mbalimbali katika kutekeleza majukumu ya kila siku. Mfumo huo unaunganisha Idara zote muhimu kwa mfano Idara ya Fedha, Idara ya Rasilimali watu, Idara ya manunuzi na nyingine.
  • Matokeo ya kukamilika kwa mfumo huo, ni sambamba na ufanisi katika uandaaji na utoaji wa taarifa za hesabu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, ambapo mfumo huo umeiwezesha TPA kupata hati safi kwa miaka miwili mfululizo kwa kaguzi zinazofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
  • Aidha, kutokana na matumizi ya mfumo huo, TPA imeweza kupata tuzo ya uandaaji bora wa taarifa za hesabu kutoka kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, NBAA.
  • Zaidi ya hayo, mfumo huo umeongeza tija pia katika kuhakikisha udhibiti wa mianya ya upotevu wa fedha, uandaaji wa taarifa mbalimbali kwa wakati, utunzaji wa nyaraka na taarifa za kifedha na rasilimali za taasisi. Kutokana na kuimarika mifumo ya ukusanyaji mapato imepelekea mapato ya TPA kuongezeka kwa asilimia 27 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2021/2022.
  • Mafanikio mengine ni kwa upande wa kuhudumia shehena ambapo kumekua na ongezeko kubwa kwa upande wa Meli na shehena ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 idadi ya Meli zilizohudumiwa na Bandari za TPA ziliongezeka na kufikia meli 4,762 kutoka meli 4,160 ambazo ni wastani wa ongezeko la asilimia 13.9 kwa mwaka.
  • Kwa upande wa shehena kiwango cha shehena kilichohudumiwa ni tani milioni 8 sawa na wastani wa ongezeko la asilimia 21.7 ya shehena iliyohudumiwa katika mwaka husika ukilinganisha na miaka ya nyuma.
  • Aidha kwa upande wa miundombinu, Mamlaka ya bandari imefanya uboreshaji mkubwa wa miundombinu ikiwemo uundwaji wa mifumo ya TEHAMA, Utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam (DMGP), Uboreshaji wa Bandari Tanga, Upanuzi wa Bandari ya Mtwara, Uboreshaji wa Bandari za Maziwa Makuu
  • Uwekezaji huo mkubwa na ununuzi wa mitambo pamoja na ujuzi kwa wafanyakazi umeongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa Mamlaka ya Bandari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

Biashara

Meridianbet Expanse Tournament ushindi rahisi  

Spread the love  Jisajili na Meridianbet kisha uwe wa kwanza kupata taarifa...

Biashara

Mbinu bora za kubeti kwa mafanikio

Spread the love  MIONGONI mwa burudani zinazidi kupata umaarufu ulimwenguni, kubeti katika...

error: Content is protected !!