Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu RC Songwe ageuka mbogo Sekondari Ileje kukosa maji, ampigia simu Meneja RUWASA
Elimu

RC Songwe ageuka mbogo Sekondari Ileje kukosa maji, ampigia simu Meneja RUWASA

Spread the love

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk. Francis Michael ameagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) mkoani Songwe, kuhakikisha Shule ya wasichana Sekondari Ileje inapatiwa huduma ya maji ndani ya siku tatu, ikiwemo kupeleka mtambo wa kuchimba kisima ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa  tatizo la ukosefu maji kwa wanafunzi shuleni hapo. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea)

Dk. Michael ametoa agizo hilo leo Jumamosi baada ya kufanya ziara kwenye shule hiyo,  kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo mawili ambayo ni  nyumba moja  ya walimu itakayotumiwa na familia mbili,  inayogharimu kiasi cha Sh milioni 100 pamoja na jengo la maktaba.

Mkuu wa Mkoa amechukua hatua hiyo, baada ya Mkuu wa shule hiyo, Valeria Haule kueleza changamoto ya ukosefu wa maji shuleni hapo, ambapo alisema inawalazimu kila siku kununua maji kutoka kwa wachuuzi.

Baada ya kupokea changamoto hiyo, Mkuu wa Mkoa alilazimika kumpigia simu Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Songwe, Mhandisi Charles Pambe na kumtaka kupeleka timu ya wataalam wa maji katika shule hiyo kwa ajili ya kupeleka mabomba yatakayotumika kutoa maji kwenye kisima kilichokuwa kikitumiwa na mkandarasi wa barabara Mpemba – Isongole hadi kuyafikisha shuleni hapo.

Mbali na kupeleka maji hayo ya kisima kwa dharura, pia Mkuu wa Mkoa alimtaka Meneja huyo wa Ruwasa kupeleka mtambo shuleni hapo kwa ajili ya kuchimba kisima kitakachomaliza kabisa tatizo hilo la ukosefu wa maji.

“Meneja umeniambia una magari matatu ya kuchimba visima yapo Tunduma, sasa nataka hadi kufika Jumapili (Novemba 5, 2023) uwe umeleta gari moja na kuanza kuchimba kisima hapa” alitoa maelekezo hayo kwa njia ya simu.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) kuruhusu moja ya nyumba zilizokuwa zikitumiwa na mkandarasi aliyejenga barabara ya Mpemba- Isongole itumike kama bweni kwa wanafunzi hao wa kike, kwani tayari Tanroad ilishatoa nyumba nyingine mbili zinazotumika kama mabweni katika shule hiyo.

Awali katika taarifa yake, Mkuu wa shule hiyo, Haule alisema bweni moja lilikuwa likilaza wanafunzi 38, hivyo kupata nyumba moja kutasaidia kupunguza msongamano, wa wanafunzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

Elimu

Janeth Mbene apongeza HKMU, ataka wahitimu wajiajiri

Spread the loveWAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), ...

error: Content is protected !!