Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Mara ashangazwa maisha duni ya wachimbaji madini
Habari Mchanganyiko

RC Mara ashangazwa maisha duni ya wachimbaji madini

Spread the love

 

SERIKALI Mkoani Mara imeshangazwa na kitendo cha Wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu wa Mgodi wa Ilasanilo uliopo Wilayani Butiama Mkoani Mara, kuishi kwenye makazi duni licha ya kumiliki mali nyingi kupitia uchimbaji wa madini hayo. Anaripoti Paul Kayanda, Mara … (endelea).

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Suleiman Mzee, amewataka wananchi wa eneo hilo kujenga nyumba imara na bora za kuishi kulingana na kipato walichonacho na siyo kuishi kwenye nyumba sizizofaa wakati wanamiliki mali zenye thamani.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea eneo lake la utawala katika Mkoa mzima wa Mara baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Mara baada ya kutengua uteuzi wa mtangulizi wake Ali Hapi.

Mzee amesema kuwa dhumuni kubwa la ziara yake ni kuyafikia maeneo yote ya wadau wa maendeleo katika Mkoa huo kujitambulisha, kuyaona na kuwaona ili asiwaache nyuma akianza kutekeleza majukumu yake ya kikazi katika kukuza uchumi wa Mkoa huo.

“Nawapa pongezi wachimbaji wadogo kuja na wazo la kuungana na kuwa kitu kimoja katika shughuli hizi za madini, lakini siwapi pongezi kwa kitu kimoja tu, hakuna maendeleo hakuna nyumba bora watu mnachimba dhahabu mnapata dhahabu ya kutosha lakini mnaishi maisha mabaya ya kwenye nyumba za muda,” amesema Mzee na kuongeza;

“Wachimbaji wasasa wakipata fedha wanawekeza kwenye makazi kwa kujenga nyumba bora, sio kama wale wa zamani waliokuwa wakipata fedha zinaishishia kwenye masuala ya zinaa lakini inashangaza kuona wachimbaji wa mgodi huu wanaishi kwenye makazi ya muda wakatiwanapata dhahabu nyingi, nyumba bora ni afya Maisha mabaya ya namna hii nikuitesa familia,” alisema.

Katika hatua nyingine katika ziara hiyo mkuu huyo wa Mkoa alionesha kutofurahishwa na utendajiwa kazi wa Mgodi wa Catamining uliopo Kijiji cha Kataryo wilayani Butiama kwakutoshiriki vizuri shughuli za jamii pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ya Afya na Maji kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

“Naagiza migodiyote ifuate utaratibu wa serikali, dosari nilizoziona zirekebishwe, tafadharindugu zangu ninyi ni wadau wa maendeleo wakubwa sasa Mgodi usionekane nitatizo, unapaswa kuwajibika ipasavyo na siyo kujengeana uadui kifupi migodi yoteya Mara hakuna kinachovutia kwenye makaratasi wapo vizuri kuonesha utekelezajiwa miradi kwa wananchi lakini ukienda kwa wananchi haionekani,” alilalamikamkuu wa Mkoa.

Ziara hiyo yamkuu wa Mkoa wa Mara Suleiman Mzee ilikuwa ni kutembelea eneo lake la utawalana kifikia wadau mbalimbali wa maendeleo, na kuanza na migodi midogo yawachimbaji wadogo na wawekezaji wa kati lengo ni kujitambulisha kwao na kuonaili kujifunza

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!