Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ratiba mazishi ya Mkapa hii hapa
Habari za SiasaTangulizi

Ratiba mazishi ya Mkapa hii hapa

Spread the love

SERIKALI imetangaza ratiba ya mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa, aliyefariki dunia usiku wa jana tarehe 23 Julai jijini Dar es Salaam, atazikwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ratiba hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wakati akizungumza na wanahabari.

Waziri Majaliwa amesema, mazishi ya Rais Mkapa yatafanyika siku ya Jumatano tarehe 29 Julai 2020, kijijini kwao Lupaso wilayani Masasi, Mtwara.

“Rais wetu pamoja na kamati ya mazishi ya kitaifa imeshaandaa ratiba nzima ya tukio hili, marehemu atakwenda kuzikwa kijiji kwake Lupaso wilayani Masasi, Mtwara,” amesema Waziri Majaliwa.

Amesema, shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Rais Mkapa itafanyika kwa siku tatu mfululizo, kuanzia Jumapili tarehe 26 Julai 2020 hadi Jumanne Julai 28 mwaka huu, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

“Siku ya Jumapili kuanzia saa nne asubuhi, dhehebu la Katoliki litaongoza misa ambayo pia Wana Dar es Salaam watapata fursa ya kuanza kuaga mwili, lakini Mtanzania yeyote atapata nafasi kuuaga mwili baada ya misa,” amesema Waziri Majaliwa.

Ameeleza “zoezi la kuuaga mwili litaendelea siku nzima, hata kama itakuwa usiku mpaka Jumatatu nayo pia siku nzima itatumika kuaga.”

Waziri Majaliwa amesema, Jumanne ya tarehe 28, 2020 ni siku itakayotumika kuaga kitaifa ambapo viongozi mbalimbali Serikali, dini na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

“Siku ya Jumanne tutaenda nayo na shughuli ya kuaga hadi saa sita mchana, na baadaye watumishi wataenda kwenye maeneo yao ya kazi, kisha saa nane mwili utaandaliwa na utasafirishwa kwenda Lupaso,” amesema kuongeza:

“…Jumatano wana Lupaso, Masasi, ndugu na jamii watapata heshima na fursa ya kuaga mwili huu mpaka saa sita kamili, saa nane mchana Jumatano mazishi yatafanyika, tumeweka saa nane ili wanaopenda mazishi wasafiri na kurudi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!