Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mhariri MwanaHALISI apenya kura za maoni Z’bar
Habari za Siasa

Mhariri MwanaHALISI apenya kura za maoni Z’bar

Jabir Idrissa
Spread the love

JABIR Idrissa, aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI, ameshinda kura za maoni za ubunge kupitia Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Pangawe, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Unguja … (endelea).

Jabir aliyekuwa mmoja wa waajiriwa wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), iliyokuwa ikizalisha magazeti ya MwanaHALISI, Mseto na Mawio amepata kura 41 dhidi ya mpinzani wake Hamad Ali Hamad aliyepata kura 36. Bahamadi alikuwa mbunge wa Magogoni, mjini Zanzibar mwaka 2010-2015.

Washindani wengine kwenye kura hizo walikuwa Aminie Mohamed Juma aliyepata kura 20 na Juma Khelef Juma aliyepata kura tano kati ya kura 103, kura moja iliharibika.

Jabir alianza kuitumikia Kampuni ya HHPL mwaka 2006 akitokea gazeti la Mtanzania.

Magazeti la MwanaHALISI, Mseto na MAWIO yamefungwa na serikali kwa kudaiwa kufanya uchochezi. Jabir alijiunga na chama hicho visiwani Zanzibar mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!