Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya RAS Songwe ashangaa ujenzi zahanati kukwama kwa miaka miaka 4
Afya

RAS Songwe ashangaa ujenzi zahanati kukwama kwa miaka miaka 4

Spread the love

Katibu tawala mkoani Songwe, Happiness Seneda ametoa siku saba kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe kupitia idara ya Afya kuanza ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya majengo kwenye Zahanati ya Msia ambao ujenzi wake ulisimama baada ya fundi kukimbia. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Seneda ametoa maagizo hay oleo Jumatatu alipofanya ukaguzi kwenye zahanati hiyo na kubaini kusuasua kwa ujenzi huo unaotegemewa na wananchi.

Amewataka viongozi wa halmashauri ya Mbozi kukaa na wasimamizi wa idara ya afya wanaosimamia mradi huo kuona mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi ndani ya siku saba ujenzi uanze.

“Haiwezekani ujenzi uanze mwaka 2019 hadi leo 2023 usikamilike ilihali ujenzi wenyewe baadhi ya sehemu hauridhishi, Serikali ilitoa fedha za ujenzi kitendo cha mradi kusua hakikubaliki,” amesema Seneda.

Awali akizungumzia hali hiyo Mganga mfawidhi wa zahanati hiyo, Amanyisye Rungwe amesema zahanati ya Msia iliyopo kijiji cha Msia, Kata ya Msia, tarehe 4 Oktoba 2021 walipokea fedha  kiasi cha Sh milioni 38 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji na usafi.

Amesema lengo la mradi ni kuongeza ufanisi wa huduma za afya ili kutoa huduma za matibabu na huduma za afya ya uzazi na mtoto, matundu sita na bafu moja na choo cha walemavu na watumishi vimejengwa.

“Baada ya kupokea maelekezo na taratibu za matumizi ya fedha hizo, shughuli za utekelezaji wa ujenzi zilianza rasmi Disemba 2021 ambapo shughuli za uchimbaji wa mashimo na chumba cha kujifungulia zilianza lakini ujenzi huo ulikwama baada ya mkandarasi kukimbia,” amesema.

Amesema baada ya mkandarasi kususia mradi walitafuta fundi mwingine ambaye alikuja na kupiga hesabu za gharama ya ujenzi hivyo wiki ijayo ataanza ujenzi.

Hata hivvyo, aliomba idaraya manununuzi waharakishe madokezo ya malipo ili waende kasi.

Mwenyekiti wa CCM kata ya Msia, Jiva Mwasenga amesema kitendo cha kusuasua mradi huo kimewaumiza wakazi wa kata hiyo hivyo ujio wa katibu tawala huyo umeleta tija.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!