Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Wajasiriamali wanawake watakiwa kujitangaza kidijitali
Biashara

Wajasiriamali wanawake watakiwa kujitangaza kidijitali

Spread the love

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amewataka wanawake na vijana nchini kutumia TEHAMA kutangaza biashara zao ili kuyafikia masoko na kutanua wigo wa biashara sambamba na kuongeza kipato. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jumuiya ya wafanyabiashara wanawake wa Kiislamu (Muslimah Boss Network) Jijini Dar es Salaam jana, Issa alisema wanawake na vijana wanatakiwa watumie zaidi teknolojia ya mitandao ya kijamii kuzitangaza biashara zao na kuteka masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Kupitia mtandao wenu mnaweza kujengeana uwezo wa namna bora ya kukuza mitaji yenu nakufanya vizuri katika biashara na kamwe msikate  tamaa. Tumieni  teknolojia ya mitandao ya kijamii kujitangaza zaidi ili kuongeza tija kwenye biashara mnazozifanyfanya,” alisema Beng’i

Beng’i alisema serikali ilishaweka wazi dhamira yake ya kuwajengea uwezo na kuwainua kiuchumi  wanawake na vijana ikiwemo kutoa mikopo kupitia halmashauri na hivyo wachangamkie fursa  zinazojitokeza kwa kujikwamua kiuchumi.

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’I Issa (watatu kulia) akifurahia jambo na washiriki wa mkutano wa Mwaka wa jumuiya ya wafanyabiashara mwanawake wa kiislamu (Muslimah Boss Network), uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. (Watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya ‘Muslimah Boss Network’, Zulfa Adam.

“Nitoe rai kwa wanawake wafanyabiashara na wajasiriamali ambao bado hawajaanza kutumia teknolojia ya mitandao ya kijamii waanze kuzitumia teknolojia hizi kufungua zaidi biashara zao na kuwafiki masoko na watu wengi kwa mara moja,” alisema.

Kuhusu mitaji, Beng’i alisema  kwa sasa kuna wigo mpana ambao umefunguliwa kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali kwa njia ya uwekezaji  ambapo   mtu anapewa mtaji  pasipo kuchukua mkopo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya ‘Muslimah Boss Network’, Zulfa Adam alisema mkutano huo wa mwaka umewakutanisha wafanyabiashara wanawake zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya nchi ikilenga kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo wa namna bora wa ufanyaji biashara na kuondokana na ufanyaji biashara wa mazoea.

“Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020 kumekuwa na mafanikio makubwa, kwani hapo awali tulianza na wanachama 10 lakini tunaona mpaka kufikia sasa tunawanachama hai zaidi ya 100,” alisema na kuongeza kuwa bado uhamasishaji unaendelea ili kuvutia wanawake wengi kujiunga na mtandao huu,” alisema Adam.

Naye, Mshiriki wa mkutano huo, Rahma Jamal  alisema kupitia jumuiya hiyo ameweza kutanua wigo wa wateja wake kutokana na elimu iliyotolewa na  wakufunzi mbalimbali na hivyo  biashara yake kuimarika.

“Kupitia jumuiya hii nimenufaika sana kwani nimepewa  mafunzo  mbalimbali ambayo yamesaidia kukuza na kutanua wigo wa ufanyaji biashara yangu. Na kupitia mkutano huu mwaka tumepewa mbinu bora za kutumia mitandao ya kijamii ili  kuwafikia wateja wengi zaidi  na kuwa na kipato endelevu, “ alisema Jamal.

Mkutano wa Mwaka wa jumuiya ya wafanyabiashara mwanawake wa kiislamu (Muslimah Boss Network), unalenga kujengeana uwezo na kukuza uelewa kuhusu biashara, za mtandaoni ikiwa na lengo la kuongeza ufikiaji wa soko na kukuza mbinu za kibiashara kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!