Spread the love

Rais wa zamani wa Honduras, Juan Orlando Hernandez amekamatwa na polisi nyumbani kwake kufuatia ombi la Marekani la kutaka kiongozi huyo apelekwa nchini humo kwa tuhuma za zinazohusiana na biashara ya dawa za kulevya na silaha. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Kukamatwa kwake kumekuja wiki tatu baada ya Hernandez kuachia madaraka na madai ya miaka kadhaa ya waendesha mashtaka wa Marekani yanayomhusisha walanguzi wa dawa za kulevya.

Jana Jumanne tarehe 15 Februari, 2022, Jaji wa mahakama ya juu ya haki nchini Honduras aliyeteuliwa kushughulikia kesi yake, alisaini kibali cha kukamatwa kwa rais huyo wa zamani.

Hernandez anatuhumiwa kula njama na makundi ya kusafirisha dawa za kulevya na ufisadi katika taasisi nyingi za umma, kuzorota kwa shughuli za kijamii na kudhoofisha matumizi ya haki nchini Honduras.

Nchi hiyo kwa sasa inaongozwa na mpinzani wa Hernandez, Xiomara Castro ambaye ni mwanamke wa kwanza kuongoza nchi hiyo.

Marekani inamtuhumu Rais huyo wa zamani kushirikiana na magenge ya uhalifu wa dawa za kulevya ambayo yalibeba maelfu ya tani za Cocaine kutoka Venezuela na Colombia kisha kuzisafirisha kuelekea nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *