RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy jana tarehe 17 Julai, 2022 ametumia amri za kiutendaji kuwafuta kazi mkuu wa idara ya usalama ya wa taifa hilo – SBU pamoja na mwendesha mashtaka mkuu nchini. Inaripoti Mitandao ya kimataifa … (endelea).
Amri ya kufukuzwa kazi kwa mkuu wa SBU, Ivan Bakanov ambaye ni rafiki wa Zelenskiyy tangu utotoni, na mwendesha mashtaka mkuu, Iryna Venediktova zilichapishwa kwenye tovuti rasmi ya rais muda mfupi baada ya hatua hiyo kuchukuliwa.
Kupitia ujumbe tofauti wa Telegram, Zelenskyy amesema kwamba amechukua hatua hiyo baada ya kubainika kwamba baadhi ya maafisa kutoka idara za wakuu hao walikuwa wakishirikiana na Russia.
Ameongeza kusema kwamba jumla ya kesi 651 za usaliti na kushirikiana na Russia zimefunguliwa dhidi ya maafisa wa usalama, huku nyingine 60 zikiwa dhidi ya maafisa kutoka ofisi za Bakankov na Benediktova.
Zelenskyy sasa ametangaza Oleksiy Symonenko kuwa mkuu mpya wa idara ya kuendesha mashitaka.
Huyu raisi anadhani vita ni mchezo. Ulaya yote iko kimya kwa sababu Urusi imeiokoa Dunia kwa kuteketeza maabara nane (8) zilizokuwa zinajaribu kutengeneza virusi kuua warusi na hata sisi waafrika.
Wananchi sasa wamemchoka, yeye ndiyo tatizo.