Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi
Kimataifa

Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi

Felix Tshisekedi, Rais wa DR Congo
Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi, amemteua aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa DR Congo kuwa waziri wa ulinzi. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ … (endelea).

Rais Tshisekedi amefanya uteuzi huo leo tarehe 24 Machi 2023 ambapo amemteua Jean Piere Bemba ambaye aikuwa kiongozi wa wahalifu katika nchi hiyo kwa kipindi kirefu. Jean alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na kufunguliwa mashitaka.

Kiongozi huyo alipatikana na hatia ya kushindwa kuwazuia wanamgambo wake kufanya uhalifu ikiwa na mauaji ya watu wasio na hatia, ubakaji na uporaji wa mali za raia.

Baada ya hapo Piere, makamu wa Rais wa zamani wa Congo aliondolewa mashtaka baada ya kukata rufaa mahakama ya Kimataifa ya uhalifu mwaka 2018.

Uteuzi wake unakuja wakati jeshi la DRC likipambana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa nchi hiyo. Nchi hiyo ya Rwanda inashirikina na wanamgambo wa M23 katika kufanya uhalifu nchini Congo kutokana na sababu za kisiasa miongoni mwa nchi hizo.

Tshisekedi pia amemteua mkuu wake wa zamani wa wafanyakazi, Vital Kamerhe, kuwa waziri wa uchumi.

Sambamba na hilo Kamerhe alipatikana na kosa la ubadhilifu wa fedha lakini akaachiliwa kwa kukata rufaa mwaka jana.

Mabadiliko hayo ya mawaziri yanakuja huku nchi hiyo ikitarajia kufanya uchaguzi wa Rais mwezi Disemba mwaka huu, Rais Tshisekedi akitarajia kuwania tena kiti hicho.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember/DREAMS”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Kagame afumua tena Jeshi, awafuta kazi maofisa zaidi ya 200 wakiwemo majenerali

Spread the love  RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, amewafuta kazi Meja Jenerali...

Kimataifa

Urusi imelipua bwawa kuu la umeme nchini Ukraine

Spread the loveSERIKALI mjini Kyiv nchini, Ukraine imeushutumu utawala wa Rais Vladimir...

Kimataifa

Rais Kagame afanyia mabadiliko makubwa jeshi, usalama wa taifa

Spread the loveRAIS wa Rwanda, Paul Kagame amefanye uteuzi wa wakuu wapya...

Kimataifa

Miili ya waliofariki kwenye ajali ya treni India, kukabidhiwa baada ya vipimo vya DNA

Spread the love  TAKRIBANI watu 260 wamefariki na wengine karibu 650 wamejeruhiwa...

error: Content is protected !!