Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa
Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Sweetbert Nkuba
Spread the love

 

MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Sweetbert Nkuba amelaani kuenguliwa kwa jina lake kwenye hatua za awali za mchakato wa uchaguzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana tarehe 23 Machi 2023, Nkuba alisema anatarajia kukata rufaa kupinga uamuzi huo uliotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TLS, Charles Rwechungura hivi karibuni.

Nkuba alieleza kuwa anazo sifa za kuwa mgombea na kwamba ameshangazwa na kitendo cha kuenguliwa kwa jina lake kwa hoja ya kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali pia hakuwahi kuhudumu shughuli za uwakili kwa muda wa miaka kumi.

“Kwa mujibu wa sheria yetu na kanuni za uchaguzi za TLS nina sifa za kugombea …kulikuwa na hoja mbili hoja ya kwanza sikuwahi kufanya kazi ya uwakili kwa miaka kumi pili niliwahi kuwa mtumishi wa serikali sababu hizo sijakubaliana nazo kwani tangu nimeapishwa kuwa wakili huu ni mwaka wa 13 au 14 ni zaidi ya miaka 10 pili ni kweli nilikuwa mtumishi wa serikali na nilishaacha kazi serikalini kwa kufuata taratibu zote za kisheria kwa hiyo kamati imetumia maneno ya fununu kutoa uamuzi lakini sitaki kueleza sababu kiundani kwa kuwa nina jopo la mawakili walionipendekeza kuwania urais wakiongozwa na Jeremiah Mtobesya hivyo jopo linafanya utaratibu wa kukata rufaa,” alisema Nkuba.

Nkuba alisema kuwa anataka kukata rufaa ili haki ionekane imetendeka lakini pia kuhakikisha uwepo wa demokrasia kwenye vyama vyote vya kitaaluma ili kitendo hicho kisijitokeze tena.

Dk. Aloyce Rugazia Wakili wa Nkuba ambaye atamwakilisha mbele ya kamati ya Rufaa ya TLS alisema kuwa kigezo kilichotumika kumng’oa mteja wake ni cha kibaguzi kwakua kufanya kazi serikalini haiwezi ikamtia Wakili dosari kiasi hicho.

“Mteja wangu alinipigia simu nikapitia uamuzi uliotolewa na kamati na nimeona kuwa kuna mambo yanahitaji ufafanuzi kwa sababu yanaibua utata kwa mfano wanasema mteja wangu alikuwa mtumishi wa serikali kwa hiyo kwa mujibu wa taarifa za TLS mteja wangu amefanya kazi ya uwakili miaka miwili wanajaribu kutoa kile kipindi alichotumikia serikali mimi naona ni ubaguzi kwa watu waliotumikia serikali,” alisema Rugazia.

Dk. Rugazia alisema kuwa watafika mbele ya kamati ya Rufaa ya TLS ili kupata tafsiri ya kufanya kazi ya uwakili kwa kipindi cha miaka kumi kuna hesabiwa kwa kigezo kipi.

“Nafikiri tafsiri ya kufanya kazi ya uwakili iangaliwe ni lini alitunikiwa cheti cha uawakili ni ni lini alikabidhiwa cheti cha uwakili nafikiri ni uamuzi unaotakiwa utazamwe upya” alisema Dk. Rugazia.

Dk Rugazia alisema kuwa rufaa yao ikigonga mwamba mbele ya kamati basi watalazimika kutoka nje kwenda Mahakama Kuu kukata rufaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!