October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Trump atikisa dunia

Donald Trump, Rais wa Marekani

Spread the love

DONALD Trump, Rais wa Marekani ameamua ‘kutangaza’ dawa ya chloroquine kuwa anaitumia kupambana na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

“Nimeamua kutumia,”Trump alisema katika mkutano wake na wanahabari na kuongeza “nimekuwa nikitumia kidonge kimoja kila siku kwa wiki moja na nusu sasa.”

Taarifa hiyo imeshtua madaktari dunia, wengi wao wamesema kinachofanywa na Trump ni kushawishi dunia kuanza kutumia dawa hiyo dhidi ya corona.

Dk. Amir Khan, mmoja wa madaktari nchini humo katika andiko lake amesema, tarehe 19 Mei 2020 amepinga ‘tangazo’ hilo na kuonesha hofu yake kwa dunia iwapo dawa hiyo itatumika kukabiliana na corona.

Trump alisema, dawa hiyo itaanza kutumika wiki hii. Uamuzi wake umeshtua wanasayansi na madaktari ndani na nje ya taifa hilo, licha ya kupingwa, amewapuuza.

Wanasayansi na watafiti hao wamehoji, Trump anapataje ujasiri wa kuitangazia Marekani matumizi ya dawa hiyo wakati haijahakikishwa na mamlaka husika?

“Tangazo kama hili ni hatari kwa watu wanaomsapoti pia watu wanaopambana kuhakikisha virusi vinapungua nchini,” ujumbe wa madaktari nchini humo umeeleza na kusisitiza, Machi 2020, raia mmoja wa taifa hilo alifariki kwa kutumia chloroquine kama dawa dhidi ya corona.

Taarifa ya madaktari hao imeeleza kwamba, chloroquine ilitengenezwa kwa ajili ya Malaria, “hata mgonjwa huanza kutumia dawa hii baada ya kupata ushauri wa daktari.”

Madaktari wamesema, matumizi ya chloroquine yanahitaji upimwaji wa damu, mapafu na ini na ndipo daktari huamua mgonjwa atumie ama la.

Wameeleza, madhara ya awali yanayoweza kumpata mtu anayetumia dawa hiyo kinyume ni pamoja na kichwa kuuma, kuwa mchovu, kukosa choo na maumivu ya tumbo.

Na kwamba, madhara makubwa ambayo pia yanaweza kutokana na matumizi ya chloroquine ni upofu, kupoteza uwezo wa kusikia, kushusha sukari mwilini, msongo wa mawazo na hata mtu kujiua.

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) imeeleza, kuangalia uwezekano wa matumizi ya chloroquine kama dawa muhimu ya kupambana na corona.

“Hata hivyo, mpaka sasa kwenye mtandao wao wanaeleza, hakuna ushahidi wowote kwamba chloroquine inatibu ama inaweza kutumika kama kinga ya corona,” wameeleza madaktari hao.

Na kwamba, Aprili FDA ilieleza “baadhi ya watu waliotumia chloroquine dhidi ya corona, wamekuwa na tatizo la mapigo ya moyo, ” wamesisitiza.

Licha ya Trump kushawishi matumizi ya chloroquine, madaktari na wanasayansi wanaendelea kusisitiza kwamba, hakuna sababu ya matumizi ya dawa hiyo na wanapinga ushawishi huo.

error: Content is protected !!