Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Tunataka kupunguza kukopa
Habari za Siasa

Rais Samia: Tunataka kupunguza kukopa

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassana, amesema Serikali yake inakwenda kupunguza kukopa fedha kwa ajili ya utekelezaji huduma za kijamii kwa wananchi, kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitatu imekopa sana. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Machi 2024, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizihamasisha halmashauri kuongeza ukusanyaji mapato, katika hafla ya uapisho wa viongozi aliowateua hivi karibuni.

“Kwa sababu tunakwenda kupunguza masuala ya kukopa hasa kwa huduma za jamii sababu katika miaka mitatu hii tumekopa sana kwa ajili ya huduma za jamii, elimu, afya, maji, umeme na mambo mengine. Sasa tunakokwenda miaka miwili hii mwaka huu na mwakani mnajua fika matumizi makubwa yataelekea wapi, ili fedha ziweze kurudi TAMISEMI lazima tufanye jitihada za kukusanya,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amesema fedha zitakazokopwa na Serikali zitaelekewa katika miradi mikubwa ya maendeleo ya kitaifa, kama miradi ya barabara, madaraja, uzalishaji umeme.

“Kuna miradi mikubwa ya kitaifa, kuna mabwawa, kuna reli hizo, madaraja makubwa, mabarabara makubwa, kuna miradi mikubwa ya kitaifa hii sasa ndiyo inatakiwa kwenda huko. Kwenu mambo ya kijamii nadhani tumefanya vya kutosha tunakwenda kupunguza fedha la sivyo mkusanye,” amesema Rais Samia.

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha hali ya uchumi kwa 2022 , mwaka jana bungeni jijini Dodoma, alisema deni la taifa limeongezeka hadi kufikia Sh. 79.1 trilioni, ambapo deni la ndani ni Sh. 51.16 trilioni wakati la nje likiwa ni Sh. 27.93 trilioni.

Rais Samia amesema halmashauri nyingi zinakosa fedha kwa kuwa zinashindwa kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha, hivyo Serikali yake itakwenda kutoa fedha kwa halmashauri kulingana na kiwango cha ukusanyaji wake.

“Lakini tunakwenda kufanya hivi, halmashauri zitapewa fedha kutokana na kiwango cha makusanyo yake, unakusanya chini ya asilimia 50 unaletewa kwa kiwango hicho . Sasa wakipiga kelele kule mimi nafanya tathimini ya utendaji wako, unataka tathimini iwe nzuri leta fedha,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!